Sibuka FM

Mkuu wa mkoa wa Simiyu ashangazwa na wahitimu wa (JWTZ) kushindwa kujitegemea.

18 October 2021, 1:30 pm

Kwenye picha ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh,David Kafulila akizungumza na vijana wa mkoa huo wakati wa kongamano la vijana lililofanyika katika ukumbi Alliance

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mh,David Kafulila ameshangazwa na kitendo cha wahitimu wa wafunzo ya (JWTZ)kushindwa kujitegemea baada ya kuhitimu mafunzo yao licha ya Serikali kutumia gharama kubwa kwa ajili ya mafuzo hayo

David Kafulila ameyasema hayo wakati wa kongamano la vijana lilililofanyika Mkoani hapo kwenye ukumbi wa Alliance,kongamano lililoandaliwa na vijana wa vyuo vikuu na wahitimu wa vyuo  mkoani hapo (Simiyu Youth Platform) akizungumzia suala hilo mkuu  huyo wa Mkoa amewakumbusha vijana falisafa ya misingi ya elimu ya kujitegemea

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh,David Kafulila akizungumza na vijana wakati wa kongamano la vijana mkoani hapo.

Kwa upande wake afisa wa maendeleo Mkoani hapa  Bw,Fadhili Wiliam,amewakumbusha vijana  kuchangamkia fursa ya mikopo ya asilimia 10% inayotolewa  na Halmashauri,mikopo  ambayo kwa sasa haina riba kwa mujibu wa marekebisho ya sheria ya mikopo hiyo ya mwaka 2018-2019 inayowataka wakurugenzi  kutenga 10% ya mapato kwenye Halmashauri zao.

Sauti ya afisa maendeleo mkoa wa Simiyu Fadhili Wiliam akizungumza na vijana kwenye kongamano la vijana.

Akizungumza na kongamano hilo kamishina wa vyuo na vyuo vikuu Nchini Bw,Sospiter Bulugu,amewakumbusha vijana kujali afya zao na kujiepusha na matumizi ya madawa ya kulevya na vileo ili waweze kuzifikia ndoto zao.

Sauti ya kamishina wa vyuo na vyuo vikuu nchini Sospeter Bulugu akiwa kwenye kongamano la vijana mkoa wa Simiyu.