Sibuka FM

Red Cross: Mwanamke ni nguzo muhimu kwa taifa

10 March 2024, 8:38 am

Picha ya Pamoja ya Wanachama wa Chama Cha Msalaba Mwekundu wakiwa katika hospitali ya wilaya ya Maswa mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kufanya Usafi katika Kusherekea siku ya Wanawake Duniani zoezi hilo limefanyika mnamo tarehe 09.03.2024 Picha na Paul Yohana

Chama cha msalaba mwekundu mkoani Simiyu kimesherekea siku ya Wanawake duniani kwa kufanya usafi katika hospitali ya wilaya ya Maswa katika kutambua na kuthamini mchango wa Wanawake katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo nchini.

Na,Paul Yohana

Katika kuenzi na kuthamini mchango wa Wanawake kwenye ujenzi nchi  duniani kote Chama cha Msalaba mwekundu Mkoa wa Simiyu  kimesherekea siku ya wanawake duniani kwa kufanya usafi katika hosptal ya wilaya ya Maswa ili kuongeza chachu na hamasa kwa wananchi na wanachama wengine hasa wanawake kujiunga na chama hicho

 Akizungumza kwa niaba ya wanachama wa msalaba mwekundu mwenyekiti wa chama hicho kutoka Kikundi Cha Upendo,Bi.Ester Lukas amewaomba wanachama hao kuwa na moyo wa kujitolea katika kuenzi siku ya Wanawake duniani ambayo hufanyika kila mwaka mnamo tarehe 08.march ili kutambua mchango wa Wanawake katika Nyanja mbalimbali.

Sauti ya Mwenyekiti wa msalaba mwekundu akizungumza mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kufanya usafi Katika hospitali ya wilaya ya Maswa

Aidha Afisa Afya wa Hospitali ya Wilaya ya Maswa Bi, Asha Muharam ameupongeza umoja wa wanachama hao kwa kujitoa kwao kwenye  jamii  hasa kwa kufanya usafi katika eneo la hospitali.

Sauti ya Afisa Afya katika hospitali ya wilaya ya Maswa akiwapongeza Wanachama hao kwa kujitoa kwao na kuwaomba waendelee na Moyo huo hata kwa Jamii Nyingine

Dkt.Boniphace Mabonesho ni Afisa Afya na mafunzo toka msalaba mwekundu amesema kuwa chama hicho kimeamua kusherehekea siku ya Wanawake dunia kwa kufanya usafi katika eneo la Hospitali ya wilaya ikiwa ni moja wapo katika kuenzi na kuthamini harakati za wanawake.

Sauti ya Afisa Afya na Mafunzo kutoka msalaba mwekundu Dkt.Boniphace Mabonesho akitoa hamasa kwa Wananchi wengine kujiunga na Chama hicho

Joseph Magembe ni mmoja wa wanachama  amewaomba wananchi ushirikiano wao na kuwaunga mkono katika kuboresha chama hicho.