Sibuka FM

Rc  Simiyu  aonya  Wanaume  wanaonyemelea  Wanafunzi  wa  Kike  na kukatiza   ndoto  zao

30 October 2023, 5:19 pm

Aliyesimama ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt Yahaya Nawanda akizungumza na Wananchi katika ziara yake Wilayani Maswa. Picha na Nicholaus Machunda

Na Nicholaus Machunda

Mkuu  wa  Mkoa  wa  Simiyu  Dkt  Yahaya  Nawanda  amewaonya  Wanaume  wote  wanaotongoza Wanafunzi  na  kuwapatia  Ujauzito   unaopelekea  kukatisha ndoto  zao  za  Masomo.

RC   Nawanda  amesema   hayo  katika  Ziara  yake  Wilayani  Maswa  ya  kukagua    Miradi mbalimbali   ya  Maendeleo  ikiwemo  Ujenzi  wa   shule  mpya  za  Sekondari   na  Msingi.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt Yahaya Nawanda
Baadhi ya Wanafunzi wa kike Wilayani Maswa

Aidha  Mkuu  wa  Wilaya  ya  Maswa  Mh Aswege  Kaminyoge  amesema  kuwa   Serikali  ya  Awamu  ya  Sita  imeleta   fedha  nyingi  katika  Kila  sekta   ambapo   katika Elimu  kata  thelanini  na  Sita  ni  kata  moja   tu  ambayo  haina  shule  ya  Sekondari.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh Aswege Kaminyoge

Paul  Maige  ni  Mwenyekiti  wa  Halmashauri  ya  Wilaya  ya  Maswa  amesema  kuwa  jumla  ya  shilingi  Bilioni  1. 5  zilimeletwa  kwa  ajili  ya  utekelezaji   wa  Mradio  wa  BOOST  ambapo  ujenzi  wa  shule   mpya   umekamilika.

Sauti ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mh Paul Maige

      Kwa upande  wake  Mwenyekiti  wa   Serikali  ya  kijiji  cha  Shinyangamwenge  kilichopo  kata  ya  Dakama   Ndugu  Deusi  Mikembo  amemshukuru  Mh  Rais  Samia   kwa  kuondoa   adha   waliyokuwa   wanapata   wanafunzi  ya  kutembea  umbali  mrefu  kwenda  shuleni.

Sauti ya Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Shinyanga mwenge – Maswa

         Mwenyekiti  huyo  ameiomba  Serikali  ifanye  Utekelezaji  na  ufuatiliaji wa  ahadi  inapokuwa  inaahidi   wananchi  ili  kujenga  uaminifu  zaidi.

Sauti ya Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Shinyanga mwenge
Muonekano wa shule Mpya mojawapo ya Sekondari zilizojengwa ambapo Mkuu wa Mkoa wa simiyu alikagua ujenzi wake