Sibuka FM

Ongezeko la mamba mto Simiyu latishia maisha ya wananchi

11 March 2024, 5:43 pm

Pichani:Afisa Wanyamapori Lusato Masinde toka kitengo cha ujirani mwema (TAWA)Kanda ya Ziwa akitoa elimu Shule ya Sekondari,Bushashi Kata ya Ipililo Wilayani Maswa Mkoani hapa kuchukua tahadhari dhidi ya Mamba.Picha na Alex Sayi

Na,Alex Sayi-Simiyu

Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania TAWA Kanda ya Ziwa, wabainisha kuwa  uwepo wa mtawanyiko wa Maji kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha kwa hivi sasa kumechangia ongezeko la Mamba mto Simiyu hivyo kuhatarisha maisha ya wananchi wanaoishi karibu na mto huo.

Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania (TAWA)Kanda ya Ziwa wametahadharisha wakazi waishio pembezoni mwa Mto Simiyu juu ya uwepo wa ongezeko la Mamba kutokana na Mvua nyingi zinazoendelea kunyesha kwa hivi sasa.

Akizungumza na Sibuka Fm Redio, Lusato Masinde Afisa Wanyamapori kitengo cha ujirani mwema TAWA Kanda ya Ziwa amesema kuwa kumekuwa na matukio ya watu kujeruhiwa au kuliwa na Mamba kutoka na ongezeko la Mamba Mto Simiyu

Sauti ya Lusato Masinde Afisa Wanyamapori

Masinde ameongeza kuwa hivi karibuni kumekuwa na matukio ya vifo vitokanavyo na  Mamba Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu na Bunda Mkoani Mara na kuwataka wazazi kuchukua tahadhari kwa watoto wao.

Sauti Lusato Masinde Afisa Wanyamapori

Innocent Kavela Kaimu mtendaji Kijiji cha Ipililo Kata ya Ipililo Wilayani Maswa Mkoani hapa amezungumzia tukio la mtoto mwenye umri wa miaka (9)Masanja Maduhu kujeruhiwa na Mamba hali iliyopelekea kifo chake.

Sauti ya kaimu Mtendaji Kijiji cha Ipililo Innocent Kavela

Aidha kwa upande wake Mwl Meckiad Ruyingo makamu Mkuu  Shule ya  Sec Bushashi amesema kuwa anaishukuru (TAWA)kwa kufika Shuleni hapo nakutoa Elimu ya kuchukua tahadhari dhidi ya mnyama huyo.

Sauti ya Kaimu Mkuu Shule ya Sec Bushashi Meckiad Ruyingo

Mariam Salumu na Dotto Mashosho wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bushashi wameishukuru TAWA kwa elimu walioipata hali ambayo itawasaidia kuchukua tahadhari dhidi ya mnyama Mamba.

Sauti za wanafunzi Sec Bushashi Mariam Salumu na Dotto Mashosho
Pichani:Lusato Masinde Afisa Wanyamapori kitengo cha Ujirani mwema (TAWA)Kanda ya Ziwa akitoa elimu