Sibuka FM

DC Maswa ataka ushirikishwaji wa sekta binafsi kuleta maendeleo

17 April 2024, 10:49 am

Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge akizungumza na wajumbe katika kikao cha baraza la biashara. Picha na Samwel Mwanga

Sekta binafsi ni mdau muhimu sana wa maendeleo katika kuwaletea maendeleo wananchi wetu, nendeni mkashirikiane nao, sikilizeni changamoto zao na kuzitatua.

Na, Daniel Manyanga 

Mkuu wa Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu Aswege Kaminyoge amezitaka sekta binafsi na sekta za umma kushirikiana kwa pamoja katika kuwaletea maendeleo eananchi wilayani hapo.

Aswege Kaminyoge ametoa rai hiyo wakati akifungua kikao cha baraza la biashara wilayani hapo kilichofanyika katika ukumbi mdogo wa mikutano na kuwakutanisha wafanyabiashara, wakuu wa sekta binafsi na wakuu wa sekta za umma kikiwa na lengo la kuona namna nzuri ya kushirikiana katika kuleta maendeleo kwa wananchi wilayani hapo.

Sauti ya DC Kaminyoge akizungumza na wadau wa maendeleo wa sekta binafsi na umma

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Maisha Mtipa amesema kuwa sekta hizo zikishirikiana kwa pamoja katika kutatua changamoto mbalimbali kila mmoja atanufaika na shughuli wanazozifanya hivyo maendeleo katika wilaya wataenda kwa Kasi zaidi.

Sauti ya mkurugenzi mtendaji ,Maisha Mtipa akiweka wazi mikakati ya kushirikiana na sekta binafsi

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya Aswege Kaminyoge ametaka fedha zote za miradi ya maendeleo zinazoletwa na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania wilayani hapo kuhakikisha asilimia kubwa ziweze kuwanufaisha Wananchi moja kwa moja ili kuleta mzunguko mkubwa wa fedha.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Maswa akitaka kuwa na uwazi Kwenye fedha zinazotolewa na serikali