Sibuka FM

Maswa:Wanawake bado niwaathiria wa vitendo vya  ukatili wakijinsia.

11 December 2023, 6:56 pm

Pichani:Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye maadhimisho ya siku (16)zakupinga ukatili wa kijinsia.Picha na Alex Sayi.

Takwimu zimeonyesha kuwa bado kuna idadi kubwa ya wanawake wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia Wilayani Maswa Mkoani Simiyu.

Na Alex Sayi.

Imebainishwa kuwa Wanawake Wilayani Maswa Mkoani Simiyu wameendelea kuwa waathirika wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa na Ofisi ya Ustawi wa Jamii Wilayani hapa.

Hayo yamesemwa na Afisa Ustawi wa Jamii Wilayani hapa Grace Mmasi  kwenye kilele cha maadhimisho ya siku (16) za kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika  Desemba 10 Mwaka huu viwanja vya Madeko Wilayani hapa kwa ufadhili wa Shirika la World Divission

Mmasi amesema kuwa kwa mujibu wa Takwimu kuanzia mwezi Januari hadi Octoba mwaka huu wanawake wapatao (626)walifanyiwa ukatili wa kijinsia Wilayani Maswa Mkoani hapa.

Sauti ya Afisa Ustawi wa Jamii (W)Maswa Grace Mmasi
Pichani:Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Maswa Grace Mmasi.Picha na Alex Sayi

Akizungumzia suala la ukatili wa kijinsia Mkuu wa kituo cha Polisi Wilayani Maswa Mkoani hapa (ASP) Mkimbu Ramadhani amesema kuwa idadi kubwa ya waathirika wa Ukatili wa kijinsia ni wanawake

Sauti ya Mkuu wa Kituo cha Polisi (W)Maswa (ASP)Mkimbu Ramadhani
Pichani:Mkuu wa Kituo cha Polisi Maswa(ASP)Mkimbu Ramadhani.Picha na Alex Sayi

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya Maswa Dkt,Hadija Zegega akizungumzia  athari zinazotokana na masuala ya ukatili wa kijinsia amesema kuwa uwepo wa vitendo hivyo unawaathiri wahusika kisaikologia,kijamii na kiuchumi.

Sauti ya Mganga Mkuu Hospitali ya (W)Maswa Dkt,Hadija Zegega

Nae Mratibu wa Mradi wa maendeleo ya Jamii  Kata ya Shishiyu Wilayani hapa Betty Isaack amesema kuwa Miradi inayotekelezwa na Shirika la World Divission Wilayani hapa imelenga kuleta usawa kwenye maeneo yasiyo na usawa.

Sauti ya Mratibu Mradi(World Divission)Betty Isaack
Pichani:Mratibu wa Mradi wa Maendeleo ya Jamii Kata ya Shishiyu toka (World Divission)Betty Isaack.Picha na Alex Sayi

Aidha kwa upande wake mgeni rasmi Venance Saria Afisa Tarafa Tarafa ya Nung’hu Wilayani hapa akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya amesema kuwa jamii inapaswa kuwekeza kupinga ukatili wa kijinsia bila kubagua jinsia ya mtu.

Sauti ya Afisa Tarafa Venance Saria
Pichani:Aliyesimama ni Afisa Tarafa Venance Saria,wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Biafra “A”Charles Seni,wa kwanza kushoto (ASP)Mkimbu Ramadhani wa pili aliyevaa miwani Mganga Mkuu Hospitali ya Maswa Dkt,Hadija Zegega anaechukua faili ni Betty Isaack (World Divission)Picha na Alex Sayi.