Sibuka FM

DC Kaminyoge atoa ufafanuzi  changamoto ya sukari wilayani Maswa

28 February 2024, 11:15 am

Mkuu wa Wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge akizungumza na Wafanyabiashara Kuhusu changamoto ya Sukari na Maelekezo ya Serikali Pamoja na Kusikiliza Kero zao na kuzitafutia Ufumbuzi ; Picha na Nicholaus Machunda

Mkuu  wa  Wilaya  ya  Maswa  Mkoani  Simiyu  Mh,  Aswege  Kaminyoge  ametoa ufafanuzi  kuhusu  Changamoto  ya  Kupanda  kwa  bei  ya  Sukari   na  kutoa  maelekezo  ya  Serikali  kuhusu  upatikanaji  wa  Bidhaa  hiyo.

Kaminyoge  amesema  hayo  wakati  akizungumza  na  Wafanyabiashara  wa  Maswa na  kusema  kuwa   baada  ya  kufanya  utafiti  alingua  kati  ya  Wafanyabiashara  wa Maduka ya  Jumla Saba  aliowatembelea  ni  Wafanyabiashara  Wawili tu ndio  Walioonyesha  Risti  za  Manunuzi  ya  Sukari kwa  Wauzaji  wakubwa.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge akizungumza na Wafanyabiashara

Mkuu huyo  wa  Wilaya   amesema  kuwa  Serikali  imeshatoa  bei  elekezi   kwa  Bidhaa  hiyo  hivyo  ni  vizuri  Wafanyabiashara  Wakawa  Wazalendo  kwa  Kufuata  bei  hiyo  ili  kuepuka  kuwanyonya  Watumiaji  ambao  ni  Wananchi  wa  Kawaida

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge akizungumza na Wafanyabiashara

Baadhi  ya  Wafanya  biashara walipaza  sauti  zao  kwa Mkuu  wa  Wilaya  na kuelezea  Kero   mbalimbali  ikiwemo   Milango  katika  Machinjjio  ya Nyama, Dampo la kutupia  Uchafu,  Vitambulisho  wa  Wajasilia mali,  Huduma  za  Matibabu  kwa  Wazee.

Sauti za Baadhi ya Wafanyabiashara Wilayani Maswa

Mkurugenzi  Mtendaji  wa  Halmashauri  ya  Wilaya  ya  Maswa   Ndugu  Maisha  Mtipa  amesema  kuwa   atatekeleza  yote  waliyokubalian  hivyo  kila  Mtu  atimize wajibu  wake  katika  kufanikisha  na  kuahidi  kufanya  kikao  kingine  kwa  kutoa  elimu  zaidi  kwa  wafanyabiashara,.

Aliyesimama ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Maswa Maisha Mtipa akitoa Ufafanuzi juu ya Hoja zilizoulizwa na Wafanyabiashara wakati wa Kikao hicho
Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Maisha Mtipa

Robert  Gunda  ni  miongoni  wa  Wafanyabiashara  katika  Soko  kuu  la  Maswa  amemshukuru  Mkuu  wa  Wilaya  kwa  kufika  na  kusikiliza  kero  za  kwani  muda  mrefu  walikuwa  hawajui  wapi  pakupekeleza  Changamoto  zao.

Sauti ya Robert Gunda Kitoa Shukurani kwa Mkuu wa Wilaya kwa kusikiliza Kero zao
Wafanyabiashara wakiwa wamekaa wanamsikiliza Mkuu wa Wilaya