Sibuka FM

Maafisa tarafa, VEO na WEO kusimamia uandikishaji wa wanafunzi Maswa

18 December 2023, 9:40 am

Pichani: Katikati mwenye suti ni Mkuu wa wilaya ya Maswa Mhe.Aswege Kaminyoge,Kulia kwake ni Mwenyekiti wa halmashauri Mhe.Paul Maige anayefata ni Meneja RUWASA wilaya Ndg.Lukas Madaha na kutoka kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Ndg.Maisha Mtipa Picha na Daniel Manyanga

Zoezi la uandikishaji wa wanafunzi wanaoanza masomo katika mwaka masomo 2024 kwa elimu ya msingi na sekondari lipo chini ya afisa tarafa, watendaji wa kata na vijiji kwa kushirikiana kwa ukaribu na wenyeviti wa vijiji na vitongoji.

Na Daniel Manyanga

Mkuu wa Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu Mhe.Aswege Kaminyoge amewataka Maafisa Tarafa,Watendaji wa kata na Vijini kuhakikisha wanasimamia ipasavyo zoezi la uandikishaji  kwa Wanafunzi wa awali na msingi pamoja kidato cha kwanza katika mwaka wa masomo 2024 masomo yatakayoanza mwezi January.

Kaminyoge ametoa Rai hiyo wakati akitoa salamu za kheri ya Krismas na mwaka mpya kwa Wafanyakazi na Wananchi wilayani hapo katika  mkutano wa Mwaka wa Wadau wa Sekta ya Maji ulioandaliwa na wakala wa Maji na usafi wa mazingira Vijijini  Wilayani hapo (RUWASA) uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya hiyo.

Kaminyoge amesema kuwa tunaelekea mwaka 2024 ambapo kunazoezi la kuandisha Wanafunzi watakao anza elimu ya msingi na awali lakini pia elimu ya sekondari kwa wanafunzi ambao wamemaliza elimu ya msingi ambapo wanatakiwa kuanza masomo mara moja pasina kuwa na kisingizio chochote kutokana na serikali ya awamu  sita ya rais Mhe.Dr.Samia Suluhu Hassan kutoa elimu bila malipo.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe.Aswege Kaminyoge akizungumza na wadau katika mkutano wa mwaka wa maji

Kaminyoge ameongeza kuwa swala la uandikishaji siyo swala la Mkuu wa Shule,Mwalimu Mkuu na wala Mkuu wa wilaya badala yake swala la kuhakikisha wanafunzi wanaandikishwa na kuanza masomo yao Msingi na Sekondari ni jukumu la Afisa Tarafa,Watendaji wa Kata na Vijiji wakishirikiana kwa ukaribu na Wenyeviti wa Kijiji na Kitongoji .

Dc Kaminyoge akitoa maagizo kwa maafisa tarafa na watendaji wa kata na kijiji kusimamia uandikishaji wa wanafunzi

Katika hatua nyingine Mhe.Aswege Kaminyoge amemuomba mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo,Maisha Mpita kukaa na Madiwani ili waweze kuona namna nzuri ya  kuwashirikisha wananchi  kuweza kuchangia ujenzi  wa miundombinu muhimu ya vyoo licha ya serikali ya awamu ya sita kuendelea kutoa fedha za ujenzi wa vyoo  katika baadhi ya shule za msingi na sekondari  ambazo zinaupungufu wa matundu ya vyoo.

Picha za pamoja za baadhi ya wadau wa sekta ya maji wakifatilia kwa makini mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ya maji wilayani Maswa