Sibuka FM

DC  Maswa  aagiza viongozi, watendaji  kusikiliza kero za wananchi

13 March 2024, 11:35 am

Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Mwabayanda Kata Ng’wigwa Wilayani Maswa wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya katika Mkutano wa Hadhara wa Kusikiliza Kero za Wananchi. Picha na Nicholaus Machunda

Mkuu  wa  Wilaya ya  Maswa  mkoa  wa  Simiyu  Mh  Aswege  Kaminyoge   ametoa  maagizo   kwa  watendaji na  viongozi  wengine  kusikiliza  kero za  za  wananchi  na kuzitafutia  ufumbuzi na  siyo  kusubiri viongozi  wa  ngazi  za  juu kuja  kusikiliza  kero  ambazo  zingetatuliwa na  viongozi  hao.

Mh Kaminyonge  ametoa  maagizo  hayo leo  katika  mkutano  wa hadhara  wa  wananchi wa wakati   wa  kusikiliza kero  za  wananchi  na  kuzitafutia  ufumbuzi  ili   wananchi  waendelee  kuiamini  serikali  yao chini  ya  Mh  Rais   Samia  Suluhu  Hassan.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh Aswege Kaminyoge

Aidha  mkuu  huyo  wa  wilaya amewataka  wazazi  na walezi  kuchangia  chakula  cha  watoto  shuleni  ili wapate chakula shuleni wawe  na  uwezo   wa  kusoma  vizuri  kwani  tafiti  zinaonesha  watoto   wanaokula  shuleni  wana nafasi  kubwa  ya  kufanya   vizuri  katika  masomo  yao  ya  darasani.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh Aswege Kaminyoge

Katika  kusikiliza  kero  za  wananchi, kero  ya  maji  ya  kunyweshea  mifugo  likaibuliwa  na   mwananchi Mahira  Miteko  ambapo  kaimu  mtendaji  wa  Mamlaka  ya  Maji na  Usafi wa Mazingira  Mjini Maswa (Mauwasa) Raphael  Mwita  amesema  watafuatilia  ndani  ya  siku  7 ili kuondoa  adha hiyo kwa wananchi

Sauti ya Kaimu Mkurugenzi wa Mauwasa – Raphael Mwita