Sibuka FM

Samwel na Godi mikononi mwa Dc Maswa kwa kukwepa kulipa kodi

19 April 2024, 11:49 am

Pichani ni Dc Maswa, Aswege Kaminyoge akizungumza na waandishi wa habari hawapo kwenye picha baada ya kukamata gari Picha na Samwel Mwanga.

Lazima tuwe wakali kwa wafanyabiashara ambao wamekuwa wanaihujumu Serikali yetu ya Tanzania kwa kukwepa kulipa kodi pale wanapouza na kununua bidhaa na kushindwa kutoa listi za mashine zenye thamani sawa na bidhaa husika.

Na, Daniel Manyanga 

Mkuu wa wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Aswege Kaminyoge ametoa onyo kwa Wafanyabiashara wilayani hapo wanaokwepa kulipa kodi pale wanaponunua au kuuza bidhaa zao kuacha mara moja tabia hiyo kwani kufanya hivyo kunalikosesha mapato Taifa letu ambayo yangeenda kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi

Aswege Kaminyoge ametoa rai hiyo mapema leo hii wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kufuatia kukamatwa kwa gari lililokuwa linasafirisha bidhaa za wafanyabiashara wilayani hapo na  mjini Musoma mkoani Mara bidhaa ambazo zilionekana hazionyeshi uhalisia wa bei kutoka kwa muuzaji

Kaminyoge ameongeza kuwa kutokana na oparesheni inayofanywa na mamlaka ya mapato nchini TRA wilayani hapo walifanikiwa kukamata gari lenye usajili wa namba T 954 BDU aina ya Fuso likiwa linasafirisha bidhaa kutoka Mwanza kwenda  Maswa na Musoma kwa wafanyabiashara ambapo listi zilionyesha baadhi ya bidhaa kununuliwa chini ya bei ambapo ni tofauti na bei halisi waliponunulia jijini Mwanza.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Maswa akitoa onyo kwa wafanyabiashara wakwepa kulipa kodi

Kwa upande wake meneja wa mamlaka ya mapato nchini TRA wilayani hapo,Lucius Theonesti amesema kuwa gari hiyo wanaishikiria kutokana na kusafirisha bidhaa kwa kutumia listi za mashine yaani EFD ambazo siyo sahihi kwani hazionyeshi thamani ya bidhaa,jina la muuzaji na mununuzi pamoja na TIN namba isipokuwa jina liliandikwa nyuma ya listi hizo.

Sauti ya meneja TRA wilayani ya Maswa akizungumza kwa nini gari hiyo wanaishikilia

Theonesti amesema kukwepa kodi kunaikosesha Serikali  mapato ambayo yangeenda kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa Wananchi .

Sauti ya meneja TRA wilayani akizungumzia madhara ya kukwepa kulipa kodi