Sibuka FM

Mkuu wa Wilaya akanusha  taarifa  za  Nyumba  112  kobomoka kufuatia  Mvua zinazoendelea  kunyesha

5 February 2024, 11:58 am

Mkuu wa Wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge akiwa Ofisini kwake.

Mkuu  wa  Wilaya  ya  Maswa, Mkoani  Simiyu  Mhe,  Aswege  Kaminyoge  amekanusha  taarifa iliyotolewa  kwenye vyombo  vya  habari   kuwa   nyumba  112  zilibomolewa  na   mvua  kubwa  iliyonyesha  Tarehe  27/01/ 2024  katika  kata  ya  Mbaragane    na  kusema  kuwa    ni  nyumba  5  tu zilizobomoka kutokaa  na  Mvua  hiyo.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh Kaminyoge

Amesema  kuwa  kwa  mjibu  wa  sheria  No  6  ya  Maafa  ya  mwaka 2022  na  kanuni  zake  imewapa   Mamlaka  Viongozi  wa  serikali   kama  Vile   Waziri  mkuu  kwa  ngazi  ya  Taifa, Mkuu  wa  Mkoa  kwa  ngazi  ya  Mkoa  na  Mkuu  wa  Wilaya  kwa  ngazi  ya  Wilaya.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh Kaminyoge

 Aidha  Mhe,  Kaminyoge  ameseammkuwa    taarifa  za  tahadhari  za  uwepo  wa  Mvua  kubwa  kwa  Mwaka  zilitolewa  mapema   ili  wananchi  waweze  kuchukua  Tahadhari  lakini   wengi  wao  hawakufanya  hivyo..

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh Kaminyoge