Sibuka FM

Mpango wa chakula mashuleni kuongeza ufaulu wa wanafunzi Bariadi

18 April 2024, 4:40 pm

Pichani ni magunia ya mahindi yaliyotolewa na Wazazi na Walezi ili kuwezesha mpango wa chakula mashuleni Picha na Daniel Manyanga

Chakula mashuleni ni swala la muhimu sana katika kukuza maendeleo ya wanafunzi kwenye ufaulu wa mitihani yao kitaifa na hivyo itapunguza utoro kwa wanafunzi mashuleni.

Na,Daniel Manyanga

Wazazi na Walezi wa wanafunzi katika shule ya msingi Imalilo iliyopo halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu wamechangia magunia 39 ya mahindi ,magunia matatu ya maharage na kiasi cha shilingi laki sita na elfu sabini na nane ili kuwezesha wanafunzi kupata uji na chakula cha mchana hatua itakayoweza kuongeza ufaulu katika mitihani ya kitaifa na kupunguza utoro.

Wakizungumza na Sibuka fm wakati wanakabidhi mahitaji hayo kwa shule hiyo Wazazi na Walezi hao wamesema kuwa wameamua kuchanga kutokana na shule hiyo kuonesha njia ya kuwapatia uji na chakula cha mchana ambapo kupitia mashamba ya shule hiyo imeweza kuvuna kiasi cha magunia 31ya mahindi ambayo yote yataenda kutumika kwenye mpango wa chakula shuleni hapo.

Sauti za Wazazi wa wanafunzi wakiwahamasisha wale ambao hawajatoa kufanya hivyo Ili kuinua ufaulu

Wakipokea mahitaji hayo Geofrey Kamugisha ni mwalimu mkuu wa shule hiyo na Peter Luhumbila mwenyekiti wa kamati ya shule wamewaomba wazazi na walezi ambao bado hawajachangia kushiriki zoezi hilo muhimu ili kuwezesha wanafunzi 1601 kupata uji na chakula cha mchana hali ambayo utaweza kupunguza utoro na kuongeza ufaulu shuleni hapo.

Sauti ya walimu mkuu na mwenyekiti wa kamati ya shule wakielezea matumaini yao

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Bariadi,Adrian Jungu amesema shule hiyo ni mfano wa kuigwa kwenye halmashauri hiyo huku mkuu wa wilaya ya Bariadi,Simon Simalenga  akitoa maagizo kwa shule zote wilayani hapo.

Sauti ya Dc, Simon Simalenga akizitaka shule zote kuanza mpango wa chakula mashuleni