Sibuka FM

Maswa wanogesha muungano kwa kutoa madawati

24 April 2024, 10:46 am

Pichani ni baadhi ya Wakuu wa Idara wakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge(mwenye Miwani) Picha na Nicholaus Machunda

Wakuu wa Idara Halmashauri ya Wilaya ya Maswa wamekabidhi Seti za Madawati Miatatu kwa ajili ya Shule za Msingi na Sekondari ili kupunguza Uhaba unaozikabiri shule hizo baada ya kujibana kwenye Bajeti za Matumizi ya Ofisi zao

Na Nicholaus Machunda

Katika  Kusherekea  Miaka  60  ya  Jamhuri  ya  Muungano  wa  Tanzania, Wakuu  wa  Idara  katika  Halmashauri  ya  Wilaya  ya  Maswa  iliyopo  Mkoani  Simiyu  Wameadhimisha  kwa  Kutoa  Madawati  kwa  Shule  za  Msingi  na  Sekondaari  yenye  thamani  ya  Shilingi  Milioni 18.

Akikabidhi  seti  hizo  za  Madawati  kwa  Baadhi  ya  Wakuu  wa  Shule  za  Msingi  na  Sekondari, Mkuu  wa  Wilaya  ya  Maswa  Mhe  Aswege  Kaminyoge  amesema  kuwa  Madawati  yanaenda  kupunguza  Uhaba  wa    Samani  na  kusisitiza  kuyatunza  ili  yadumu  kwa  ajili  ya  kizazi  kijacho

Sauti ya DC Maswa Aswege Kaminyoge akikabidhi Madawati

Mh  Kaminyoge   amewapongeza  Wakuu  wa  Idara hao  kwa  kujibana  katika   bajeti za  Ofisi  zao  na  kununua  Madawati  na Kutoa  Wito  kwa  Taasisi  zingine  kwenye  Ofisi  zao kutenga  Bajeti  ili  kurudisha shukurani  kwa  Jamii   kuchangia  Miundo mbinu mingine kama  Madawati  ili kufanya  wanafunzi  wasome  bila   shida  yoyote..

Sauti ya DC Maswa Aswege Kaminyoge akikabidhi Madawati
DC Maswa akikagua Madawati kabla ya kuyakabidhi kwa Wakuu wa Shule

Akimkaribisha  Mkuu  wa  Wilaya,  Kaimu  Mkurugenzi    Mtendaji  wa  Halmashauri  ya  Wilaya  ya  Maswa   ambaye  pia  ni  Mkuu  wa  Idara  ya  Ardhi    Ndugu  Vivian Christian  amesema  kuwa  Madawati  hayo  yanaenda  kupunguza  changamoto  ya   uhaba wa Madawati  kwa  baadhi  ya  Shule

Sauti ya Kaimu DED Maswa Vivian Christian

Mwl  Fedelis  Apolinary  ni  Afisa  Elimu  Sekondari  Wilayani  hapa  amesema  idara  yake  imepata  Madawati Mia mbili  ambapo  yatapelekwa  katika  Shule  za   Sekondari  Nyongo  na  Sayusayu   ambazo zilibainika  kuwa  na  Uhaba  Mkubwa    huku  akiahidi  awamu  nyingine  kupeleka  katika  shule  zingine.

Sauti ya Afisa Elimu Sekondari Fedelis Apolinary

Akitoa  Ufafanuzi  wa  Utengenezaji  wa  Madawati  hayo, Mkuu  wa   Chuo  cha  Ufundi  Stadi  Binza  Mwalimu  Mabula  Skampamu  Daniel   amesema   Madawati  hayo  wameyatengeneza  kwa  Ubora  wa  hali  ya  Juu  hivyo  yatadumu  kwa  Muda  Mrefu huku  akitoa  Rai  kwa  Wadau  na  Taasisi  mbalimbali kujitokeza kutengeneza  ili  kusaidia  Wanafunzi .

Sauti ya Mkuu wa Chuo cha Veta Binza- Mabula Skampam