Sibuka FM

CHADEMA Simiyu yajipanga kuingia  kwa  kishindo uchaguzi serikali za mitaa

25 February 2024, 6:14 pm

Pichani ni baadhi ya Viongozi wa Chadema Mkoa wa Simiyu wakiwa na Mwenyekiti ( Mwenye kalamu anayeandika) Musa Onesmo. Picha na Nicholaus Machunda.

Chama cha  Demokrasia  na  Maendeleo   Chadema  Mkoa  wa  Simiyu  kimesema  kuwa  kimejipanga  kuingia  kwa  kishindo  katika  uchaguzi  wa  serikali  za  mitaa utaofanyika  mwishoni  mwa  mwaka  huu  wa  2024.

Kauli  hiyo  imetolewa  na  Mwenyekiti  wa  Chama  hicho  Mkoa  wa  Simiyu   Musa  Onesmo  wakati  akizungumza  na  waandishi  wa  habari  kuhusu  uamuzi   wa  chama  hicho  kushiriki  katika  chaguzi  zijazo za serikali.

Sauti ya Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Simiyu Musa Onesmo

Aidha  Mwenyekiti  huyo  wa  Chama  cha  Demokrasia  na   Maendeleo   Chadema  Mkoa  wa  Simiyu amewahamasisha  Wanachama  na   Wananchi ujitokeza  kwa  Wingi  kushiriki  Maandamano  ya  Amani  hivyo  Wajiandae  kupokea  Maandamo  Mkoani  hapa.

Sauti ya Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Simiyu Musa Onesmo

Onesmo amesema  kuwa  Kupanda kwa  gharama  za  Maisha  kunapelekea  Ugumu  wa  Maisha  kwa  Wananchi  hasa  kwa  Bidhaa  Muhimu  ikiwemo  Sukari  ambapo kuipata  hadi  Upange  Foleni  au  kuuziwa  kwa  Kufahamiana.

Sauti ya Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Simiyu Musa Onesmo