Sibuka FM

CCWT kuanza usajili wafugaji kwa njia ya kielektronik

19 November 2023, 5:37 pm

Pichanini baadhi ya wafugai wakiwa mnadani, mnada wa Kidinda Bariadi Simiyu. Picha na Alex Sayi

Chama Cha Wafugaji Taifa (CCWT) ziarani nchi nzima kuhamasisha wafugaji kujisajili kwa njia ya kielektronik ili wafugaji hao wawe na chombo cha kuwaunganisha na kutatua matatizo yao.

Na Alex Sayi.

Chama Cha Wafugaji Taifa kimeendelea na ziara nchi nzima kwa lengo la kuwahamasisha wafugaji na Wakulima kujiunga na chama hicho kwa kufanya usajiri kwa njia ya Kieletronic

Kusundwa Wamalwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Wafugaji Taifa amesema kuwa (CCWT) kinaendelea na kampeni nchi nzima ya kuhakikisha wafugaji na wakulima wanajisajili ili waweze kutambuliwa na serikali na kuwa na tqkwimu sahihi za mifugo.

Sauti ya Makamu Myenyekiti (CCWT)Taifa Kusundwa Wamalwa

Wamalwa akizungumzia baadhi ya changamoto zinazowakabili wafugaji amesema kuwa kilimo kimekuwa chanzo kikubwa cha uharibifu wa mazingira licha ya watalaam kudai kuwa ng’ombe zinachangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira.

Pichani:Aliyesimama ni Makamu Mmwenyekiti(CCWT) Kusundwa Wamalwa,wapili ni Leton Leboy mjumbe Kamati tendaji Bagamoyo,mwenye Suti ni Dkt,Christopher Nzela Mratibu(CCWT) wa tatu mwisho ni Sylivery Buyaga Katibu masidizi(CCWT)na kushoto mwisho ni Sululu Dongoyu.Picha na Alex Sayi
Sauti ya Makamu Mwenyekiti(CCWT)Kusundwa Wamalwa

Nao baadhi ya Wafugaji Wilayani Maswa Mkoani Simiyu wamezungumzia baadhi ya changamoto zinazowakabili Wafugaji hao,Ngasa Sanyangi amesema kuwa kumekuwa na dhana potofu kuhusiana na Chama hicho cha Wafugaji.

Sauti ya Mfugaji na Mkulima Mkazi wa Mwawayi Kata ya Nyalikungu Ngasa Sanyangi

Akitolea ufafanuzi wa Suala hilo Sylivery Buyaga Katibu Masidizi (CCWT) Kanda ya Nyanza na Afisa Idara ya Sheria (CCWT)Makao Makuu Dodoma alisema kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Chama hicho kinasema kuwa (CCWT)haijihusishi na masuala yoyote ya kisiasa.

Sauti ya Katibu Msaidizi(CCWT)Kanda ya Nyanza na Afisa Idara ya Sheria(CCWT) Makao Makuu Dodoma Sylivery Buyaga
Pichani:Katibu Masidizi (CCWT)Kanda ya Nyanza na Afisa Idara ya Sheria(CCWT)Makao Makuu Dodoma akiwa ameshikilia moja ya kadi za Kielektronic.Picha na Alex Sayi

Dkt,Christopher Nzela Mratibu na Katibu wa Migogoro(CCWT)amewaomba wafugaji na wakulima wajiunge na Chama hicho ili Chama kiwe na nguvu ya kuwasemae Wafugaji hao pindi migogoro inapojitokeza

Sauti ya Dkt,Christopher Nzera Mratibu na Katibu wa Migogoro(CCWT) Makao Makuu Dodoma
Pichani:Kushoto Bi,Mahuma akijiandikisha kwa nia ya mtandao,katikati ni Ibrahim Kilassa,Masfirishaji na mtaalamu wa Tehama(CCWT).Picha na Alex Sayi