Sibuka FM

DC Simalenga elimu ya mikopo kwa vijana itolewe

30 July 2026, 17:15

Pichani ni mkuu wa wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga akiwa kwenye moja wapo ya kazi ya kiserikali wilayani hapo Picha kutoka maktaba ya Sibuka fm

“Tunahitaji kuona kundi la vijana wanajisimamia wao kiuchumi na siyo kuanza kulaumu serikali kwamba haitoi ajira wakati tayari serikali kupitia halmashauri kuna asilimia kumi ya mapato ya ndani inawasubiri wao ili kujikwamua kiuchumi kupitia vikundi”. 

Na,Daniel Manyanga 

Mkuu wa wilaya ya Bariadi mkoni Simiyu, Simon Simalenga amewataka maafisa maendeleo ya jamii kuanzia ngazi ya kata na halmashauri  kuhakikisha wanatoa elimu kwa vijana ili wachangamkie fursa mbalimbali zilizopo katika wilaya hiyo ambazo zinaweza kusaidia kundi hilo kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jukwaa la vijana katika halmashauri ya mji wa Bariadi,Simon Simalenga amesema kuwa wilaya hiyo inazo fursa mbalimbali ambazo zinaweza kuwanufaisha vijana hivyo ni muhimu kutolea kwa elimu na umuhimu wa fursa hizo.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga

Iddi Ndabhona ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Bariadi amesema kuwa halmashauri hiyo inaendelea kufanya jitihada mbalimbali za kuwafikia vijana na kuwaelimisha ili waunde vikundi vitakavyowawezesha kupata mikopo inayotolewa na halmashauri kupitia mapato yake ya ndani.

Sauti ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Bariadi

Baadhi ya vijana wenye ulemvu akiwemo Enock John, Krypton Mmanga na Alex Mwaisumo wameiomba serikali kuongeza ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu kwenye fursa mbalimbali na kwamba hata wao wanaweza kutoa mchango wenye tija kwenye jamii.

Sauti ya watu wenye ulemavu wakiomba ushirikishwaji