Sibuka FM

Watoto wawili wa familia moja wafariki kwa kifusi,mmoja aokolewa

21 August 2026, 20:45

Pichani ni muonekano wa kifusi kilichoondoa uhai wa watoto wa familia moja waliokuwa wakichimba mchanga mtoni Picha na Anita Balingilaki

Mzazi ni mlinzi wa kwanza kwa watoto katika kuhakikisha yupo salama sasa haiwezekani mzazi hujuwi mwanao anashinda wapi na anacheza katika mazingira yapi”.

Na,Daniel Manyanga 

Watoto wawili wa familia moja waliokuwa wakiishi katika mtaa wa mji wa zamani kata na wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, wamefariki dunia na mtoto mmoja waliyekuwa naye akiokolewa baada ya kufukiwa na kifusi cha udongo na mchanga walipokuwa wakichimba mchanga mtoni.

Tukio hilo limetokea Agosti 20, 2026 majira ya saa 10 jioni na kusababisaha vifo vya watoto hao waliojulikana kwa majina ya Bakari Rajab (8) na Salum Rajab (6) huku Rachel Rajab (8) akiokolewa kutoka kwenye tukio hilo na hapa mtoto huyo anaeleza hali ilivyokuwa hadi wao kufukiwa na kifusi hicho wakiwa mtoni.

Sauti ya manusura wa tukio

Kwa upande wake mama mzazi wa watoto hao waliofariki dunia Swaum Mgema, na bibi yao Taabu Juma, wameeleza walivyopokea taarifa kuhusiana na tukio hilo huku kijana aliyekwenda kuwaokoa akieleza hali aliyoikuta eneo la tukio.

Sauti ya wazazi na shuhuda

Mwenyekiti wa mtaa huo, Said Mapesa amesema kuwa matukio ya watu kufariki dunia kwa kufukiwa na kifusi katika eneo hilo yamekuwa ya kujirudia rudi licha ya jitihada zinazofanywa na uongozi wa mtaa huo kudhibiti watu wasifanye shughuli za uchimbaji mchanga katika eneo hilo, na kuiomba serikali iongeze nguvu za udhibiti wa watu kuchota mchanga katika eneo hilo.

Sauti ya mwenyekiti

Kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Simiyu mrakibu msaidizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji, Faustin Mtitu, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba limesababishwa na uzembe wa wazazi kutokufatilia mienendo ya watoto wao na kujuwa mazingira.

Sauti ya kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Simiyu