Sibuka FM
Sibuka FM
8 August 2026, 13:51

“Tunahitaji kutiana moyo kwa mambo yote ili kuendelea kulitangaza neno la Mungu kwa mataifa yote bila kujali hali zetu za kimwili”.
Na,Daniel Manyanga
Wito umetolewa kwa kanisa la waadventista wasabato nchini kuwatambua wamama wajane(wamama majasiri) kwa kuwasaidia vitu mbalimbali ikiwa pamoja na neno la Mungu kama njia ya kuwatia moyo baada ya kufiwa na mwenzi wao.
Wito huo umetolewa na leo hii na mchungaji, Daniel Gamal Budo wa kanisa la waadventista wasabato mtaa wa Gasuma wakati wa makambi katika kanisa la Luguru Ginnery lililopo mtaa wa Itilima kanda ya Luguru Ginnery baada ya waumini wa dini hiyo kuwakumbuka wajane(wamama majasiri) wapatao 42 wa mtaa huo na kuongeza kuwa Yesu Kristo alikufa kwa ajili ya watu wenye dhambi.
Mchungaji Budo amesema kuwa wamama wajane (wamama majasiri ) wamepokea zawadi mbalimbali ikiwemo,Vitenge,Sabuni na Fedha Taslimu ikiwa ni sadaka ya kuwakumbuka wajane hao waliofiwa na mwenza wao na kwamba kufanya hivyo ni ishara ya upendo kwa majasiri hao ambao wamesimama na Yesu Kristo licha ya kuondokewa na mwenzi wao.

Philipo Kamba Buluba ni mchungaji wa kanisa la waadventista wasabato mtaa wa Itilima amewashukuru viongozi wote walifanikisha makambi hayo katika mtaa huo kwa namna ambavyo wamejitoa kwa hali na mali.
Kwa upande wake,Wilda Petro Nyuma akizungumza kwa niaba ya wamama wajane(wamama majasiri ) waliopokea misaada hiyo amesema kuwa jambo walilofanya waumini wa kanisa la waadventista wasabato mtaa wa Itilima kanda ya Luguru Ginnery ni lakuigwa kote katika kuujenga ushirika wa Yesu Kristo kwa kuwakumbuka mashujaa hao.
Nyuma ameongeza kuwa licha ya kufiwa na mwenzi wao lakini bado wameendelea kusimama na Mungu katika mambo yote bila kuteteleshwa na maneno ya watu.
Makambi ya kanisa la waadventista wasabato mtaa wa Itilima kanda ya Luguru Ginnery wilayani Itilima yalianza rasmi mnamo tarehe 02.08.2026 hadi 08.08.2026 na kuhudhuriwa na makanisa manne ya mtaa huo ambayo ni Luguru Ginnery, Luguru Central, Zone na Ilaba pamoja wageni kutoka sehemu mbalimbali.
