Sibuka FM

Jaccafo yafanya maadhimisho ya watu wenye ulemavu Maswa

6 December 2023, 8:27 pm

Pichani:Aliesimama ni Mkurugenzi wa (JACCAFO) Joseph Ngeleja Jidayi kulia ni Katibu wa (JACCAFO)Mkoa Roseana Sewangi,kushoto Abel Cherehani Afisa Elimu,Elimu Maalumu Wilaya Maswa wa pili kushoto ni Mwenyekiti (JACCAFO)Mkoa Lucia Christian akiteta jambo na Mhazini (JACCAFO)Mkoa Nyamizi Shija.Picha na Alex Sayi

Jamii wilayani Maswa imeaswa kuwafichua watoto wenye ulemavu waliofungiwa majumbani ili waweze kuzifikia ndoto zao kielimu, kiuchumi  na kijamii.

Na Alex Sayi

Shiriki lisilo la kiserikali la Juniors and Child Care Foundation (JACCAFO) limefanya maadhimisho ya siku ya walemavu Duniani kwa mara ya kwanza Wilayani Maswa Mkoani Simiyu, lengo ikiwa ni kuihamasisha jamii ya watu wenye ulemavu kushiriki shughuli za kijami.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Shirika hilo Joseph Ngeleja Jidayi kwenye maadhimisho  ya siku ya watu wenye ulemavu Duniani yaliyofanyika Desemba 04/mwaka huu Shule ya Msingi Binza Wilayani Maswa Mkoani hapa.

Sauti ya Mkurugenzi wa (JACCAFO) Joseph Ngeleja Jidayi

Awali kabla ya maadhimisho hayo maafisa wa Shirika hilo walitembelea baadhi ya Wodi kwenye Hospitali ya Wilaya Maswa nakutoa misada mbalimbali kwa watoto,kwa wajawazito nakwa wazazi waliojifungua watoto njiti.

Sauti ya Mkurugenzi wa (JACCAFO) Joseph Ngeleja Jidayi

Dkt,Hagai Timothy Mganga mfawidhi Hospitali ya Wilaya Maswa Mkoani hapo aliushukuru uongozi wa (JACCAFO)kwa msaada walioutoa  nakuuomba  uongozi wa Shirika hilo kuielimisha jamii hasa kinamama wajawazito kuona umuhimu wa kuhudhuria Clinik

Pichani:Mganga Mfawidhi Hospitali ya Wilaya Maswa Dkt,Hagai Timothy
Sauti ya Mganga Mfawidhi Dkt, Hagai Timothy

Kwa upande wake mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo  Saguda Sayayi  Afisa Tarafa Tarafa ya Sengerema Wilayani hapa akizungumza kwa niaba ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya amesema kuwa watoto wenye ulemavu wana haki sawa na watoto wengine.

Sauti ya Saguda Sayayi

Akisoma taarifa fupi ya kitengo cha watoto wenye mahitaji maalumu Mwl,Christopher Makongo amesema kuwa kitengo kilianzishwa mwaka (2006)kikiwa na wanafunzi wanne hadi sasa kitengo hicho kinajumla ya watoto  kumi na tano

Pichani:Mwl,Christopher Makongo Mwalimu kitengo maalum Shule ya Msingi Binza.Picha na Alex Sayi
Sauti ya Mwl,Christopher Makongo

Gange Bukwimba mkazi wa kijiji kwa Igwata Kata ya Nyabubinza Wilayani hapa ametoa shukrani zake kwa Shirika hilo kwakumsaidia mwanae kupata msaada wa kiti mwendo huku akizungumzia adha alizokuwa akizipata mwanae kabla ya kupata msaada huo.

Sauti ya mzazi Gange Bukwimba
Pichani:Mtoto mwenye ulemavu Monica Ibrahim aliyefadhiliwa kiti mwendo na (JACCAFO)akiwa kwenye picha ya pomoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Binza.Picha na Alex Sayi.