Sibuka FM

DC Maswa atahadharisha wanaotorosha  mazao ya nafaka

7 February 2024, 1:56 pm

Baadhi ya wadau wa kilimo wakiwa katika mkutano wa kujadili mfumo wa Stakabadhi gharani

Mkuu  wa  Wilaya  ya  Maswa  mkoa  wa  Simiyu  Mhe  Aswege  Kaminyoge  amewatahadharisha  Wafanyabiashara  wa  Mazao ya  Nafaka utoroshaji  na  kukwepa  kulipa  Ushuru  wa  Mazao  hayo.

Mhe  Kaminyoge  amesema  hayo  katika  kikao  cha  Wadau  wa Kilimo  na  Mazao  Mchanganyiko  kilichofanyika  Katika  ukumbi  wa  Halmashauri hiyo.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge

Paul  Maige  ni  Mwenyekiti  wa Halmashauri  ya  Wilaya  ya  Maswa  amesema  kuwa mfumo  huu  wa  Stakabadhi  gharani  ni  Mzuri  maana  utamnufaisha  Mkulima moja kwa moja  na  Halmashauri  pia.

Sauti ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Maswa Paul Maige

Kwa  Upande  wake  Mwenyekiti  wa  Chama  kikuu  cha  Ushirika  Mkoa  wa  Simiyu (SIMCU )   Lazaro   Walwa  amesema  kuwa  wao  wamejiandaa  kikamilifu  kwenye  zoezi  hilo  ambalo  lina  lengo  la  Kumkomboa  Mkulima  mdogo  wa  Maswa  na  Mkoa  wa  Simiyu.

Sauti ya Mwenyekiti wa SIMCU Lazaro Walwa

Baadhi ya  Wafanyabiashara  wa  Mazao  mchanganyika  hapa  Maswa  wamepaza  sauti  zao  kwa Mkuu wa Wilaya kuhusu  changamoto  zilizojitokeza  katika  Misimu  iliyopita   Halmashauri  wamejipangaje  kwa  Mfumo  huu  Mpya wa  ununuzi wa  mazao  kwa  njia ya Stakabadhi  gharani.

Sauti ya Baadhi ya Wafanyabiashara wa Mazao mchanganyiko