Sibuka FM

Wakulima Maswa waaswa kutumia mbegu bora zilizofanyiwa utafiti

9 August 2023, 4:03 pm

Pichani: wa nne kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Maswa Maisha Mtipa akiwa na baadhi ya wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya Maswa kwenye kipando cha zao la Karanga kwenye maonyesho ya Nane nane Nyakabindi Bariadi Simiyu.Picha na Alex Sayi.

Wakulima Wilayani Maswa Mkoani Simiyu wahamasishwa kutumia mbegu bora zilizofanyiwa utafiti ili kuongeza uzalishaji kwenye sekta ya kilimo.

Na,Alex Sayi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu Maisha Mtipa amewaasa Wakulima Wilayani hapa kutumia mbegu zilizofanyiwa utafiti ili kilimo hicho kiwe na tija kwa Wakulima hao.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi huyo  kwenye kilele cha siku kuu ya nane nane iliyofanyika maeneo ya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Sauti ya Mkurungezi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Maisha Mtipa.

Mkurugenzi huyo ameongeza kwa kumshukuru Rais Samia kwa kuwekeza fedha nyingi kwenye sekta ya Kilimo,huku akiwataka Wanawake na Vijana kujishirikisha na kilimo ili sekta hiyo iwe na tija kwa wakulima hao.

Sauti ya Mkurugenzi wa Halmashauri Maswa Maisha Mtipa.

Pichani:Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Maisha Mtipa,katikati ni Mkuu wa Divission ya kilimo,Mifugo na Uvuvi Robert Urasa wakiwa na Masuke Balele Bwana Shamba toka Kampuny ya Advanta wakiwa kwenye kipando cha zao la Alzet kwenye maonyesho ya Nane Nane Bariadi.Picha na Alex Sayi

Mkuu wa Division ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi Wilayani hapa Robert Urasa Alisema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa inaendelea na mkakati wa kuwahamasisha Wakulima kulima zao la Alzet ambalo nimkombozi kwa Wakulima.

Sauti ya Mkuu wa Divission ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi Wilayani Maswa Robert Urasa

Kwa upande wake Masuka Balele Afisa kilimo  wa Campuny ya Advanta toka Mkoani Arusha ambao niwasambazaji wa mbegu hizo Mkoani hapa amewaasa Wakulima,kutumia mbegu hizo kwakuwa zinahimili hali ya hewa Mkaoni Simiyu.

Sauti ya Bwana Shamba toka Kampuny ya Advanta Masuke Balele

Aidha Salome Charles Mkulima mwezeshaji amesema kuwa kilimo cha mbengu za kisasa zilizofanyiwa utafiti zimewasaidia wakulima hao kupata mazao mengi ikilinganishwa na mbengu za kienyeji.