Sibuka FM

23 kizimbani kwa kesi ya ugaidi Mwanza

27 July 2026, 13:13

Pichani ni baadhi ya watuhumiwa wa kesi ya ugaidi wakiwa kwenye viunga vya mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mwanza wakiwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi Picha kutoka maktaba ya Sibuka fm

“Tunahitaji nchi ya amani ili kila mtu aweze kufanya shughuli zake za maendeleo bila kuwa na hofu sasa wanapotokea watu au kikundi wanapanga njama ovu hakuna aliye juu ya sheria lazima sheria ichukuwe nafasi yake”.

Na,Daniel Manyanga 

Watu 23 wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza na kusomewa shtaka moja la kushiriki kwenye mikutano ya kigaidi.

Waliopandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi ni Alphaxad Nyamwaga (57), Fantson Mpango (49), Abely Mwesa (62), Hassan Said (43), Emmanuel Wambura (30), Adam Idd (23), Damas Sadock(31), Petrol Mabula (40), Abdul Kagwidi (28), Devid Mahendeka (20), Philipo Masatu (31), Edward Mikindo (28) na Emmanuel Doto (26).

Wengine ni Deus Masalago (41), Mohamed Tosha (37), Fabian Nguvumali (52), Samwel Mtani (45), Samwel Kobell (40), Julius Makonga (34), Fanuel Lutana (35), Philipo Kulwa (37) , Philipo Shipuluko (50) na Hamis Mnyivua (35).

Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Julai 4, na Julai 7 mwaka huu, katika sehemu tofauti tofauti wilaya za Nyamagana na Ilemela mkoani humo ambapo vyombo vya ulinzi na usalama vilifanikiwa kujuwa mpango huo muovu wa kigaidi.