Sibuka FM

Huu hapa mkakati wa seriali katika kuinua zao la pamba

12 May 2026, 19:02

Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba ya Pamba Tanzania- Renatus Luneja akizungumza wakati wa uzinduzi wa msimu wa pamba 2026/2027.Picha na Nicholaus Machunda

Lazima mkulima ashiwe mkono kama mtoto mdogo anavyoshikwa mkono wakati wa kuvukishwa barabarani, ndio maana serikali inamhudumia kuanzia pembejeo hadi kwenye masoko, tunatamani heshima ya pamba urudi. ” Agrey Mwanri -balozi wa pamba tanzania “

Imeelezwa  kuwa  Serikali ya  awamu ya sita imeendelea   kuweka  mikakati mathubuti  ya kuhakikisha inasaidia  wakulima wa zao la  Pamba na kuleta tija kwa kuongeza uchumi wa mtu  mmoja mmoja

Hayo yamesemwa na Mkuu wa  Wilaya  ya  Igunga  Mhe  Sauda  Mtondoo aliyemwakilisha  Mkuu wa  Mkoa  Tabora  Mhe  Paul  Chacha   wakati  wa  Uzinduzi wa  Msimu  wa  ununuzi wa  zao  pamba  uliofanyika  katika  kijiji cha mwamashimba  wilayani  hapo ambapo bei elekezi  ya  Serikali kwa msimu huu ni  shilingi 1,240 kwa  Kilo moja

sauti ya Mhe Sauda Mtondoo DC Igunga akizungumzia mikakati ya Serikali

Kwa upande wake Kaimu mwenyekiti wa  Bodi ya  Pamba  Tanzania –TCB  na  Balozi wa  Pamba  nchini   Agrey  Mwanri  amesema  kuwa  ni  wakati  muafaka  wa  kuleta  heshima  ya  zao la  Pamba  na  kuacha  alama  kwa  wakulima  wanaolima zao hilo

sauti ya Agrey Mwanri- Balozi wa pamba Tanzania akizungumzia mikakati

Anamringi  Macha  ni Mkuu  wa  Mkoa  wa Simiyu  amesema  kuwa   mkoa wa  simiyu umekuwa  kinara kwa  uzalishaji huku matarajiwa katika  msimu huu wa  2026/2027 ni kuvuna  pamba  ya zaidi ya  kilo milioni 177  sawa na asilimia  60 ya pamba  yote  nchini  itayonunuliwa

Sauti ya Mhe Anamringi Macha mkuu wa mkoa wa Simiyu akizungumzia uzalisha wa pamba

Nao  baadhi ya  wadau wa  zao la  Pamba  wakawahakikishia  wakulima uhakika wa  Fedha  baada ya  kuuza  pamba  yao  huku  wakala  wa  vipimo  akiwaonya wale wanaofanya udanganyifu wa  kuchakachua mizani  kwa  lengo la kuwaibia  wakulima

Sauti za baadhi ya wadau wa pamba wakizungumza waati wa uzinduzi wa msimu wa pamba 2026/2027