Sibuka FM

Mvua yageuka kilio kwa wakulima wa pamba Bariadi

29 April 2024, 5:41 pm

Pichani ni muonekano wa zao la pamba kwa wakulima kutokana na kuathiriwa na mvua. Picha na Daniel Manyanga.

Licha ya mvua kuwa na faida lakini kwa wakulima wa pamba Bariadi imegeuka kilio hadi kufikiria kulima mazao mengine ili kujikomboa kiuchumi kutokana na mavuno ya pamba kuwa chini msimu huu.

Na, Daniel Manyanga 

Wakulima wa zao la pamba halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu wamelia na mvua inayoendelea kunyesha kuharibu  zao hilo hatua itakayopelekea uzalishaji kushuka na hivyo kutokufikia malengo yao katika msimu huu wa kilimo cha zao hilo.

Wakizungumza na Sibuka FM kwa nyakati tofauti, Daud Mashimo na Nkuhi Simiyu  wamesema kuwa kutokana na mvua kuwa kubwa mavuno yatashuka kutokana na zao hilo kutohitaji  mvua za juu ya wastani ambapo kwa hekari moja walitarajia kupata tani moja ambapo kwa sasa wanaweza kupata labda 200kg kutokana na mashamba kujaa maji.

Sauti ya wakulima wa pamba wakielezea matazamio ya mavuno kushuka

Issa Mtweve ni Mkuu wa Idara ya Kilimo na Uvuvi  halmashauri ya  mji wa Bariadi amekiri uwepo wa changamoto hiyo ambayo inaenda kupunguza kiwango cha uzalishaji wa zao hivyo kushuka  kwa asilimia 25.

Sauti ya afisa kilimo na uvuvi akizungumzia kushuka kwa mavuno

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bariadi,Simon Simalenga amesema kuwa maeneo ya bondeni ndiyo yameathiriwa  na wingi wa mvua hivyo kuleta  changamoto kwenye uzalishaji kwa msimu huu kutokana na mvua kuzidi.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Simon Simalenga

Katika hatua nyingine Simon Simalenga amewataka wakulima wawe wabunifu kwa kulima mazao mengine kutokana na mvua hizi zinazoendelea kunyesha ili kuweza kujikomboa.

Sauti ya DC wa Bariadi Simon Simalenga