Sibuka FM
Sibuka FM
12 December 2024, 20:59

“Suala la lishe ni mtambuka bila ushirikiano wa jamii na wadau hatuwezi kumaliza utapiamlo kwenye jamii yetu”.
Na, Daniel Manyanga
Katika kupambana na utapiamlo mkoani Simiyu halmashauri za wilaya ya Maswa na Meatu zimepokea mbegu za mahindi na maharage lishe kutoka Harvest Plus chini ya mradi wa Reacts In wenye lengo la kumaliza suala la lishe duni .
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo hii wakati wa kukabidhi mbegu hizo, Kaimu Mratibu wa mradi wa Reacts In, Esther Simfukwe amesema kuwa mbegu hizo zinapelekwa moja kwa moja kwa wakulima lengo likiwa ni kukabiliana na lishe duni huku kila kaya ikitarajiwa kunufaika na robo heka ya Mahindi na Maharage lishe msimu huu wa kilimo.

Akipokea mbegu hizo afisa kilimo wilaya ya Maswa ,Masalu Lusana amesema kuwa mbegu hizo zinaenda kugawiwa kaya masikini wenye kipato cha chini ili kusaidia kupambana na Utapiamlo unaotokana na lishe duni kutokana na familia masikini kutokuwa na bajeti za kukidhi lishe bora.
Kwa upande wake afisa kilimo wa wilaya ya Meatu ,Jesca Shedrak ametaja sababu za wilaya hiyo kuwepo katika mradi wa Reacts In wenye lengo la kumaliza swala la Utapiamlo.

