Sibuka FM

Kamati ya siasa Maswa yaridhishwa utekelezaji miradi ya maendeleo

2 December 2023, 7:44 am

Katikati mwenye Kofia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Maswa Onesmo Makota, kushoto ni Katibu wa ccm Maswa John Melele na mkono wa Kulia ni Mashimba Ndaki Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi wakiwa katika Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo inayoletwa na Rais wa Awamu ya sita Mhe, Samia Suluhu Hassan.

Kamati  ya Siasa ya  chama  cha  Mapinduzi   (CCM) Wilaya  ya  Maswa  ikiongozwa  na  Mwenyekiti wa  Chama  hicho   Ndugu  Onesmo   Makota Imetembelea   na  Kukagua  Miradi  mbalimbali  ya  Maendeleo inayotekelezwa  katika  Jimbo  la  Maswa  Magharibi.

Miradi  iliyotembelewa  na  kukaguliwa  na  Kamati  hiyo  ni  Ujenzi  wa  Tanki  la  Maji  katika  Mji  wa  Malampaka, Ujenzi  wa  Zahanati  Nyabubinza,  Mradi  wa   Umeme  Vijijini (REA), Mradi  wa  Maji  Mwatumbe na  Matengenezo  ya  Barabara  kutoka  Malampaka  hadi  Mwanh’onoli  na  Kuridhishwa  na  Miradi  hiyo.

Sauti ya Mwenyekiti wa ccm Wilaya ya Maswa Ndg Onesmo Makota

Akitoa  taarifa  ya  Utekelezaji  wa Mradi  wa  Ujenzi  wa  Tanki   la  Maji  katika  Mji  wa  Malampaka  Mkurugenzi  wa  Mamlaka  ya  Maji  na  Usafi  wa  Mazingira  mjini  Maswa (MAUWASA )  Mhandisi  Nandi  Mathias  amesema  kuwa    mradi  huo  wa  dharura  utanufaisha   Wakazi  zaidi  ya  Elfu  kumi  na tatu.

Sauti ya Mkurugenzi wa MAUWASA Mhandisi Nandi Mathias

Naye  Mbunge  wa  Jimbo  la  Maswa   Magharibi  Mhe,  Mashimba  Ndaki  amewataka  MAUWASA   kukamilisha  haraka  mradi  huo  ili  kuondoa  changamoto  ya  Upatikanaji  Maji  katika  mji  huo  ambao  unakua  kwa  Kasi  sana.

Mhe, Mashimba Ndaki Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi akisisitiza Jambo kwa Wananchi kuhusu utunzaji wa Miradi ya Maendeleo.
Sauti ya Mbunge wa Maswa Magharibi Mhe, Mashimba Ndaki

Ikiwa  katika  kata  ya  Shishiyu  kijiji  cha  Mwatumbe  kamati  ya  Siasa imekagua   chanzo  cha   maji kilichojengwa  na  RUWASA kupitia  mdau  wa  Maendeleo  WORLD VISION   na  kushauri  kuwa  Jumuiya   za  watumia  Maji  kupewa  Elimu  zaidi   juu  ya  Uendeshaji    na  Utunzaji  wa  Mradi  huo  kwa  ajili  ya  vizazi  vijavyo  na   hapa  katibu  wa  ccm  Wilaya  ya  Maswa  ndugu  John  Melele  anaeleza..

Sauti ya Katibu wa CCM Wilaya ya Maswa Ndg, John Melele

Nao  baadhi  ya  Wananchi  Wameishukuru  Serikali  ya  awamu  ya  sita  chini  ya  Mh  Rais  Samia  Suluhu  Hassan    kwa  kuleta  miradi  ambayo  imesaidia  kuondoa changamoto  walizokuwa  wanazipata  hapo  awali..

Sauti za baadhi ya Wananchi wakizungumzia kuhusu miradi ya Maendeleo