Sibuka FM

Wadau: Miaka 60 ya muungano, Maswa haikuwa hivi

27 April 2024, 10:32 am

Pichani aliyesimama ni Athumani Kalaghe Katibu Tawala Wilaya ya Maswa na Mwenyekiti wa Sherehe za Muungano akifungua Kongamano la Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya Mhe, Aswege Kaminyoge. Picha Na Nicholaus Machunda

Kongamano la Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuwa Tanzania limefanyika Katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa na Kuhudhuriwa na Wadau Mbalimbali

Nicholaus Machunda

Wadau  wa Maendeleo  Wilayani  Maswa  Mkoani  Simiyu  Wamesema  kuwa  Miaka  60  ya  Muungano  wa  Tanganyika  na  Zanzibar  na  Kuunda  Jina  la  Tanzania Umekuwa  na  Mafanikio  Makubwa  na  Umerahisisha  Upatikanaji wa Huduma  kwa  Wananchi.

Akihutubia  katika  Kongamano  lililofanyika  Katika  Ukumbi  wa  Halmashauri  ya  Wilaya  ya  Maswa, Mkuu  wa  Wilaya  hiyo  ambaye  ndie  alikuwa Mgeni  Rasmi  katika  Sherehe  hizo   Mhe,  Aswege  Kaminyoge  asema  kuwa  Maswa  ya  sasa  siyo  kama  ile  ya  Miaka  ya  Nyuma.

Sauti ya DC Maswa Mh Aswege Aswege Kaminyoge

Kamiyoge  amesema  katika  sekta   mbalimbali  mabadiliko  Makubwa  yamefanyika  na  Wananchi  wamesogezewa  Huduma  kwa  Ukaribu  zaidi  ikilinganishwa  na  hapo  awali  ambapo  Wananchi  walikuwa  wanasafiri  Umbali  Mrefu  Kufuata  Huduma  Muhimu  za  Kibinadamu.

Sauti ya DC Maswa Mh Kaminyoge

Akitoa  Ufafanuzi  wa  Maadhimisho  hayo  ya  Miaka  60  ya  Muungano,  Mwenyekiti  wa  Sherehe  hizo  ambaye  pia  ni  Katibu  Tawala  wa  Wilaya   Athuman  Kalaghe  amesema lengo la Muungano  lilikuwa  zuri  hivyo  ni  vizuri  kuenzi  na  Kuuudumisha.

Sauti ya DAS Maswa Athuman Kalagh

Mzee  Sospeter  Msuluja  ni  Mwalimu  Mstaafu  amesema  amesema  zamani  hali  haikuwa  kama  ilivyo  sasa  kwani  Maendeleo  yanaonekana kila  Kona   na  Kuwataka  Watumishi  Waliko makazini  Waendelee  Kuwatumikia  Wananchi  kwa  Ueledi  Mkubwa  na  Uzalendo.

Sauti ya Mzee Sospeter Msuluja – Mzee Mtaafu

Aidha  Kongamano  hilo  limehudhuriwa  na  Wadau  mbalimbali  Wakiwemo  Wakuu  wa  Taasisi   na  Wanafuzi  kutoka  Shule za  Msingi  na  Sekondari   nao  wakawa  na  haya  yakusema  kuhusu  Miaka  60  ya  Muungano.

Sauti za Wadau mbalimbali wa Maendeleo
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Binza Wameshiriki katika Kongamano hilo na Kuelezea Ushuhuda wa Mafanikio ya Miaka 60 ya Muungano