Sibuka FM

Maswa: RC aagiza hoja zote za CAG  zifungwe

22 June 2023, 7:13 pm

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt Yahaya Nawanda ameuagiza

uongozi wa wilaya ya Maswa kuhakikisha wanafunga hoja zote

za Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) zilizotolewa

baada ya kufanya ukaguzi wa fedha kwa mwaka wa fedha

2021/2022.

Dkt Nawanda ametoa maagizo hayo wilayani Maswa wakati wa

kikao cha Baraza Maalum la kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti

wa Hesabu za Serikali (CAG) huku akitoa siku kumi (10) kwa

halmashauri ya wilaya ya Maswa kulipa madeni ya fedha za

wastaafu kwenye mifuko ya jamii ili waweze kupata mafao yao..

Sauti ya RC Simiyu Dkt Yahaya Nawada

Aidha   Dkt  Nawanda  amesema  kuwa  Halmashauri  ya  Maswa  imekuwa  ya  Mwisho  katika  Ukusanyaji  wa  Mapato ikilinganishwa  na  Halmashauri  zingine  za  Mkoa  wa  Simiyu  huku  akiwataka  Wakuu  wa  Idara  kubuni  vyanzo  vya  Mapato  vitakavyosaidia  kuongeza  ukusanyaji  wa  Mapato na kufikia  Malengo  iliyojipangia..

         Sauti ya RC Simiyu Dkt Yahaya Nawad

Akiwasilisha taarifa ya ukaguzi wa hoja za CAG kwa mwaka wa

fedha 2021/2022, mkaguzi wa nje wa hesabu za serikali za mitaa

mkoa wa Simiyu Gwamaka Mwakyosi amesema kuwa halmashauri

ya wilaya ya Maswa imepata hati safi hivyo waendelee kufuata

taratibu zote za uendeshaji wa halmashauri ili kuepuka kupata hati

chafu..

Sauti ya Gwamaka Mwakyosi

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Maswa Mhe, Paul Maige

amesema kuwa watazingatia ushauri wote uliotolewa na ofisi ya

Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali ili kuhakikisha

wanaondoa hoja zote na kutoruhusu hoja mpya ambazo zinaweza

kuwachafulia hata.

Sauti ya mwenyekiti wa Halmashauri Paul Maige

Aswege Kaminyoge ni mkuu wa wilaya ya Maswa amesema kuwa

anajivunia kufanya kazi na madiwani kwani amekuwa akipata

Ushirikiano wa kutosha katika kuwaletea maendeleo wananchi wa

Maswa.

Sauti ya DC Maswa Aswege Kaminyoge

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya madiwani wenzake, diwani

wa kata ya Zanzui hapa Maswa Mhe. Jeremia Shigala maarufu kwa

jina la Makondeko amesema kuwa anawashukuru viongozi

waliotoa mapendekezo ya namna ya kuboresha usimamizi na

ukusanyaji wa mapato.

Sauti ya Diwani kata ya Zanzui Jeremia Shigala