Sibuka FM

DC  Kaminyoge:  Elimu ya Kisheria  iendelee  kutolewa kwa Wananchi   

1 February 2024, 8:09 pm

Katikati Waliokaa mwenye Miwani ni Mkuu wa Wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge akiwa na Wadau wa Mahakama leo katika Kilele cha Wiki ya Sheria kilichofanyika katika Viwanja vya Mahakama ya Wilaya ya Maswa.. Picha na Nicholaus Machunda

Mkuu  wa  Wilaya  ya  Maswa   Mkoani  Simiyu  Mhe,  Aswege  Kaminyoge  amewataka  wadau  wa  Sheria   kuendelea  kutoa  Elimu  kwa  Wananchi  kwani  wanawategemea  sana  katika  Utoaji  wa  Haki.

Hayo  ameyasema  katika  kilele  cha  Wiki  ya  Sheria  katika  Viwanja   vya  Mahakama  ya  Wilaya  ya  Maswa  na  Kusema  kuwa  kila  kiongozi  akitimiza   wajibu  wake  Wananchi  watakuwa  na  Furaha na  kuona  Mahakama  ndio  kimbilio  la  kupatikana   haki  ya  kila  Mtu.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe, Aswege Kaminyoge

Mh  Kaminyoge  amesema  kuwa Serikali  ina  viongozi    ngazi  zote  lengo  kuu  ni  kumsaidia  Mhe,  Rais  katika  majukumu  ya  kuwatumikia  wananchi   na  kuhakikisha   wanapata  huduma  zote  za  msingi    na  Mazingira  wezeshi.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe, Aswege Kaminyoge

Akitoa  Hotuba  ya  kilele  cha  Wiki  ya  sheria,   Hakimu  Mfawidhi  wa  Mahakama  ya  Wilaya  ya  Maswa   Mh,  Enos  Misana  amesema  kuwa  Mahakama  ndio  chombo  pekee  cha  Utoaji  wa  Haki  kikatiba   kwa  kuongozwa  na  Dira  yake.

Sauti ya Enos Misana Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Maswa
Enos Misana Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Maswa

Mh  Misana   ameongeza  kuwa   katika  wiki  ya  sheria  wamekuwa  na  jukumu  la  kuelimisha  Wananchi  kuhusu  masuala mbalimbali  yahusuyo  sheria,  shughuli  za  Kimahakama,  kupokea  maoni  na  Mapendekezo  ya  wananchi.

Sauti ya Enos Misana Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Maswa

Kwa  Upande  wake  Mwendesha  Mashitaka  Wilaya  ya  Maswa   Mhe,   Suzani   Masule  amesema  kuwa  Mahakama  pekee  haiwezi  kutoa  haki  bila  kushirikisha  Wadau  wengine  wanahusika  katika  Utoaji  wa  Haki.

Sauti ya Suzan Masule, Mwendesha Mashitaka Wilaya ya Maswa