Sibuka FM
Sibuka FM
8 August 2026, 12:51

“Matamanio yetu ni kuona watu wanabadili nia na kumgeukia Mungu maana mambo ya kidunia mara nyingi mwisho wake huwaga ni mbaya sasa ni muda mwafaka wa kuihubiri injili ya Bwana kwa watu wote”.
Na,Daniel Manyanga
Watu 54 wamebatizwa katika makambi ya mtaa wa Luguru Ginnery Kanda ya Luguru Ginnery wilayani Itilima mkoani Simiyu kufuatia kukubali kuwa Yesu Kristo ni mwokozi wa maisha yao.
Akizungumza na Sibuka Fm wakati wa kuhitimisha sikukuu ya vibanda katika makambi hayo Kanda ya Luguru Ginnery mchungaji wa kanisa la waadventista wasabato mtaa wa Gasuma ,Daniel Gamal Budo amesema kuwa ni furaha kubwa kuona watu wameamua kuachana na maisha ya dunia hivyo kumpokea Yesu ili awe kiongozi wao.
Mchungaji Gamal amewakumbusha wale wote waliopokea ubatizo wa maji marefu katika makambi hayo kusonga mbele kwa nguvu katika kuifanya kazi ya Mungu bila kujali jamii itawaonaje kutokana na ubatizo huo.
Jacob Mwampamba ni Mchungaji wa kanisa la waadventista wasabato mtaa wa Somanda wilayani Bariadi ametoa wito kwa makanisa ya mtaa wa Luguru Ginnery kuendelea kuwapa masomo wale wote waliobatizwa ili kuendelea kukaa kwenye mwokovu.

Ezekiel Magembe ni mmoja wapo wa vijana waliobatizwa katika makambi hayo amewaomba vijana wengine kuachana na anatha za dunia na kumgeukia Yesu Kristo aliyekufa msalabani kwa ajili ya watu wenye dhambi na kufanyika mkombozi hivyo wabatizwe.

Kwa upande wake meneja wa makambi kanda ya Luguru Ginnery, Manjale Magembe amesema kuwa katika makambi hayo jumla ya makanisa manne yanayounda mtaa wa Luguru Ginnery yameshiriki kwenye makambi hayo yaliyoambatana na matembezi.



