Sibuka FM

Kishindo cha miaka 65 ya magereza chaacha tabasamu kwa watoto njiti

23 August 2026, 06:19

Pichani aliyesimama ni mkuu wa wilaya ya Maswa,Dkt.Vicent Naano Anney akizungumza jambo katika maadhimisho ya miaka 65 ya magereza wilayani hapo kulia kwake ni mkuu wa gereza wilayani hapo Mrakibu wa magereza (SP),Omary Mbwambo Picha kutoka maktaba ya Sibuka fm

“Magereza siyo sehemu ya mateso kama ambavyo watu wengi wamekaririshwa na baadhi ya watu hapa ukija kama mfungwa siku unaachiwa unatoka na ujuzi ambao utakusaidia huko maana yake hii ni sehemu kurekebisha tabia na kupatiwa ujuzi”.

Na,Daniel Manyanga 

Katika kuadhimisha miaka 65 ya jeshi la magereza Tanzania bara baada ya uhuru jeshi la magereza wilayani Maswa mkoani Simiyu limefanya matendo ya huruma katika hospitali ya wilaya ya Maswa kwa kuwambuka watoto njiti pamoja na wamama waliojifungua kwa upasuaji ikiwa ni ishara ya kurudisha fadhila kwa jamii na kuimarisha uhusiano.

Picha ya pamoja ya jeshi la magereza wilaya ya Maswa pamoja mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya hiyo Picha kutoka maktaba ya Sibuka fm

Akizungumza na kipindi hichi  mkuu wa gereza wilaya wa Maswa,mrakibu wa magereza (SP) ,Omary Mbwambo amesema maadhimisho ya miaka 65 ya magereza Tanzania bara yamewapa fursa ya kwenda moja kwa moja kwa wananchi na kushiriki shughuli zenye manufaa kwa jamii.

SP),Mbwambo amesema kuwa jeshi la magereza wilayani hapo katika kuadhimisha miaka 65 wamefanya matendo ya huruma kwa watoto njiti pamoja na wamama wliojifungua kwa upasuaji na kuongeza kuwa magereza siyo sehemu ya mateso bali ni sehemu ya kurekebisha tabia na kufundisha stadi za kazi ili wakiondoka waweze kujitegemea.

Sauti ya mkuu wa gereza la Maswa,SP Omary Mbwambo

Dkt.Deogratius Mtaki ni mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Maswa amesema kitendo cha jeshi la magereza wilayani hapo kuadhimisha miaka 65 kwa kufika hospitalini hapo na kuwakumbuka watu wenye uhitaji ambao wanahitaji faraja ni jambo la kuigwa na taasisi zingine ili kudumisha upendo.

Mtaki ameongeza kuwa  hospitali hiyo ina wagonjwa ambao uwezo wao wa kujihudumia ni mdogo hivyo kupitia misaada iliyotolewa na jeshi la magereza kitawasaidia katika kipindi ambacho wanaendelea na matibabu pamoja uangalizi kwa watoto njiti.

Sauti ya mganga mfawidhi
Pichani ni mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Maswa, Dk Deogratius Mtaki aliyevalia tsheti nyeupe akizungumza jambo baada ya kupokea msaada wa watoto njiti kutoka jeshi la magereza wilayani Maswa Picha kutoka maktaba ya Sibuka fm

Akipokea misaada hiyo kwa niaba ya watoto njiti muuguzi wa wodi ya watoto njiti na wamama wa upasuaji,Grace Mandonde amelishukuru jeshi la magereza kwa kuwagusa watoto njiti kutokana na kuhitaji mahitaji kila siku hivyo ni ngumu kumudu gharama hizo kwa baadhi ya wahanga huku mmoja wapo wa waliofikiwa misaada hiyo ,Salome Ibrahimu amelishukuru jeshi la magereza kwa kuwakumbuka katika kipindi hichi kigumu na kuziomba taasisi zingine za kiserikali na binafsi kuiga mfano huo kwa kuwakumbuka watu wenye uhitaji.

Sauti ya muuguzi
Pichani ni muuguzi wa wodi ya watoto njiti, Grace Mandonde akipokea misaada kwa niaba ya wazazi ambayo imetolewa na Jeshi la magereza wilayani hapo katika kuadhimisha miaka 65 ya magereza Tanzania bara baada ya uhuru Picha kutoka maktaba ya Sibuka fm

Maadhimisho ya miaka 65 ya jeshi la magereza Tanzania bara baada ya uhuru yalipamba na michezo ya kuvuta kamba kwa wanaume na wanawake,kukimbia na gunia,kukimbiza kuku,kutembea na yai kwenye kijiko,mchezo wa rede ,mashindano ya kula na buruduni ya muziki wa kizazi kipya na asili huku vitu vilivyotolewa ni sabuni za kufulia, mafuta ya kupaka, pampasi za watoto,mafuta ya nazi