Sibuka FM

Maswa:Ukatili wa kijinsia watajwa kupungua

12 December 2024, 15:51

Pichani:Kulia ni mwenyekiti wa kijiji cha Mbugamita Kata ya Senani Wilayani hapa Tuju Ndungati Matalu,akifuatiwa na Katibu tawala Wilaya ya Maswa Athmani Kalaghe,kushoto mwisho ni Rodgers Limo Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya jamii Wilaya ,wakiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa wa shirika la World Vision.Picha Alex Sayi.

Wadau na wanaharakati wa haki za binadamu Duniani  na Nchini Tanzania wameendelea na harakati za kuhakikisha kuwa usawa kwa wote unafikiwa,licha yakuwepo na wimbi la taarifa za ukatili wa kijinsia unaoripotiwa kwenye maeneo mengi Nchini na Duniani kwa ujumla.

Na,

Alex Sayi

Halmashauri Wilayani  Maswa Mkoani Simiyu imebainisha kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia vinaonyesha kupungua kutoka matukio(671)mwaka 2023 hadi kufikia matukio(591)2024.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Ustawi wa jamii Wilayani hapa Bi,Lilian Clement kwenye kilele cha maadhimisho ya siku(16) za kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyikia kijiji cha Mbugamita kata ya Senani Wilayani hapa.

Sauti ya Afisa Ustawi wa jamii Wilaya ya Maswa Bi,Lilian Clement
Pichani:Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Maswa Bi,Lilian Clement.Picha na Alex Sayi

Dr,Stanford Kaserwa Meneja mradi wa (React-in)akizungumza kwenye warsha hiyo amesema kuwa shirika limeendelea kuwahamasisha vijana wa kiume na kinababa kushiriki mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia

Pichani:Dr,Stanford Kaserwa Meneja Mradi wa (React-in)Picha na Alex Sayi
Sauti ya Dr,Stanford Kaserwa
Pichani:Kulia ni Magreth Charles, afisa toka shirika la World Vision,akifuatiwa na Dr,Stanford Kaserwa Meneja Mradi wa (React-in)toka shirika la World Vision,akifuatiwa na Sifania Amos na kushoto mwisho ni Bi,Herieth Yusuph toka World Vision.Picha na Alex Sayi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa,Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bw,Athmani Zahoro Kalaghe amesema kuwa Serikali ilishatunga Sheria na miongozo, hivyo jamii inapaswa kutoa taarifa pindi tu wanapobaini kuwepo kwa matukio hayo.

Sauti ya Katibu Tawala Wilaya ya Maswa Bw, Athman Zahoro Kalaghe
Pichani:Ni Katibu tawala Wilaya ya Maswa Bw,Athman Zahoro Kalaghe
Pichani:Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku(16) za kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika kijiji cha Mbugamita Kata ya Senani Wilayani hapa.Picha na Alex Sayi