Sibuka FM
Sibuka FM
12 May 2026, 18:00

Yamezungumzwa mengi na watangulizi wangu lakini naomba nikuongezee machache mgeni rasmi kuwa hapa Igunga kutajengwa kiwanda kiubwa cha kuchakata pamba kabla ya mwaka huu haujaisha maana tayari tumeshapata eneo “Renatus Luneja Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya pamba Tanzania-TCB “
Serikali kupitia Bodi ya Pamba Tanzania TCB imetangaza bei elekezi ya ununuzi wa zao la Pamba kwa msimu wa 2026/ 2027 ambapo Pamba ya daraja la kwanza itanunuliwa kwa shilingi 1,240 kwa kilo moja huku pamba ya daraja la pili ikinunuliwa kwa shilingi 620 kwa kilo moja.
Bei hiyo elekezi imetangazwa na Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe Sauda Mtondoo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe Paul Chacha wakati wa Uzinduzi wa msimu wa ununuzi wa pamba uliofanyika katika kijiji cha Mwamashimba Wilayni Igunga Mkoani hapo

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania Renatus Luneja amesema kuwa kwakutambua umuhimu wa Wilaya ya Igunga Serikali itaendelea kuboresha mazingira kwa kujenga kiwanda cha kuchakata mbegu kabla ya mwaka huu kuisha
Baadhi ya wakulima waliozungumza na Sibuka wakatoa maoni yao kuhusu bei elekezi iliyotangazwa na Serikali huku wito ukitolewa kwa wakulima kuhakikisha wanazingatia utunzaji wa Pamba wakati wa Uvunaji ili kuepuka kuchafua pamba hali itayopelekea kushuka kwa thamani ya zao hilo
Bei ya pamba imeongezeka ikilinganishwa na bei ya msimu uliopita wa 2025/2026 ambapo kilo moja ya pamba ilinunuliwa shilingi 1,150 na kwa msimu huu wa 2026/2027 kilo moja ya pamba itanunuliwa kwa shilingi 1,240 sawa na ongezeko la shilingi 90 kwa kilo moja

