Sibuka FM

Maswa usalama wa mtoto siyo jukumu la walimu pekee

22 April 2024, 11:36 am

Picha ya pamoja ikiwaonyesha watoto wakiwa katika maadhimisho ya miaka 25 ya compassion katika kanisa la T.A.G mjini Maswa Picha na ,Daniel Manyanga

Usalama wa mtoto siyo jukumu la walimu wala mamlaka zinazohusika na maswala hayo wazazi ni nguzo muhimu sana katika kuyatengeneza maisha ya mtoto na kumwandalia misingi iliyo bora ili kuweza kukomesha vitendo vya ukatili dhidi yao.

Na, Daniel Manyanga 

Katika kuhakikisha Watoto wanakuwa salama wazazi na walezi wilayani Maswa mkoani Simiyu wametakiwa kushiriki kikamilifu katika kutengeneza kizazi chema  hali ambayo itapunguza au kumaliza kabisa vitendo vya ukatili kwa watoto.

Hayo yamesemwa mapema leo hii na David Ntinginya kaimu mtendaji mkuu wa mamlaka ya mji mdogo Maswa ambaye alikuwa mgeni rasmi  katika maadhimisho ya miaka 25 ya shirika la compassion ompassion international Tanzania maadhimisho yaliyofanyika katika ukumbi wa kanisa P.A.G lililopo mtaa wa Unyanyembe mjini hapo.

Ntinginya amesema kuwa usalama wa mtoto unaanza na mzazi mwenyewe kuanza kumlea katika misingi ambayo ni mizuri na siyo kuziachia mamlaka ambazo zinahusika na watoto ikiwemo walimu wa shule za msingi au sekondari .

Sauti ya David Ntinginya akiwakumbusha wazazi kuhusu ulinzi wa mtoto

Masanja Mshandete na Bertha John ni baadhi ya wazazi waliohudhuria maadhimisho hayo ambapo wamesema kuwa compassion imefanyika mkombozi katika  maisha yao kwani bali ya kuwawezesha wanafunzi lakini hata Wazazi nao wamekuwa wanawezeshwa fedha za mitaji ili kuweza kuanzisha biashara mbalimbali lengo likiwa ni kuondokana na utegemezi.

Sauti ya wazazi waliohudhuria maadhimisho ya miaka 25 ya compassion

Awali wakisoma risala kwa mgeni rasmi kwa niaba ya wanafunzi wanufaikaji wa compassion ,Salome Raphael na Anna Daud  wamesema kuwa wanafundishwa ujuzi mbalimbali katika vituo hivyo na kuomba baadhi ya majengo katika shule ya msingi Binza yafanyiwe ukarabati kwani yamekuwa chakavu.

Sauti ya wanafunzi wanufaikaji wa compassion wakiomba ukarabati wa majengo shule ya msingi Binza

Kwa upande wake Flavian Ignatus na Edward Mkudiso  waratibu wa huduma ya mtoto katika vituo vya T.A.G na Angalikana wamesema kuwa katika kupambana na ukatili kwa watoto wameanzisha mfumo wa namna bora wa kuripoti matukio ya ukatili dhidi ya watoto ili kuweza kukomesha vitendo hivyo pamoja na kuwafundisha ujuzi mbalimbali wa watoto hao.

Sauti ya waratibu wa huduma ya mtoto shirika la compassion.

Maadhimisho ya miaka 25 ya shirika la compassion international Tanzania yameenda pamoja na zoezi la upandaji miti katika shule ya msingi Binza yenye jengo la wanafunzi wenye mahitaji maalumu.