Sibuka FM

Baraza la madiwani laridhia kuvunjwa mamlaka ya mji mdogo Maswa

18 February 2024, 3:43 pm

Aliyesimama ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mh Paul Maige, Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Maswa wakiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani Robo ya Pili ya Mwaka wa Fedha 2023/2023 Mjini Maswa. Picha na Nicholaus Machunda

Na Nicholaus Machunda

Baraza  la  Madiwani  la  Halmashauri  ya   Wilaya ya  Maswa  kwa Kauli  moja  limeridhia  kuvunjwa  kwa  Mamlaka  ya  Mji  mdogo  Maswa  kwakushindwa  kukidhi  vigezo  na  Kuazimia  kuanzisha  Mchakato  wa  Kupata  Halmashauri  mbili.https://maswadc.go.tz/

Azimio  hilo  lilitolewa    na  Mkrugenzi  Mtendaji  wa  Halmashauri wa  Wilaya  ya  Maswa  Ndugu  Maisha  Mtipa  katika  kikao cha  Baraza  la  Madiwani  Robo  ya  Pili  ya  Mwaka  wa  Fedha  2023/2024  na  Wajumbe  wa  Kikao hicho kuridhia   azimio  hilo na  kuruhusu  kuanzisha  mchakato wa  Halmashauri  nyingine.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Ndugu Maisha Mtipa

Paul   Simon Maige  ni  Mwenyekiti  wa  Halmashauri  ya  Wilaya  ya  Maswa Mkoani  Simiyu   amesema  kuwa  kumekuwa  na  gharama  kuwa  za  uendeshaji  wa  Mamlaka  ya  Mji   mdogo  hivyo  kupelekea   kuipa  Mzigo  halmashauri  ya  Wilaya  kwani  Mamlaka  hiyo  ilishindwa  kujiendesha  kwa  mapato  yake

Sauti ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mh, Paul Maige

Aidha  Mhe,  Maige   amesema  kuanzishwa  kwa   Halmashauri  mbili  katika   wilaya  moja  itasaidia  kusogeza  kuduma  kwa   Wananchi   pamoja na  kuongeza  ajira  kwa  Vijana  kwani   kutakuwa na Ongezeko  la  maeneo  ya  kiutawala  na  nafasi mbalimbali  zitahitaji    Watu.

Sauti ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mh, Paul Maige

Kwa  upande  wake   Mwenyekiti  wa  Chama  cha  Mapinduzi   Wilaya  ya  Maswa   Ndugu   Onesmo  Makota  amesema  uamuzi  uliofanywa  na  Waheshimiwa  Madiwani  ni  Mzuri  kwani  unalenga  kusogeza  huduma  kwa  Wananchi  kama  ilivyo  azima  ya  Mh  Rais   Samia.

Sauti ya Mwenyekiti wa ccm Wilaya ya Maswa Ndugu Onesmo Makota

Mmoja  wa  Diwani  wanaounda  Mamlaka  ya   Mji  mdogo  Maswa    Masanja  Mpiga  asema  wamefikia  Uamuzi  huo  kutokana  na  Kkushindwa  kukidhi  vigezo  kwa  Muda  mrefu  toka  kuanzishwa  Mamlaka  hiyo  Miaka  Kumi  iliyopita.

Sauti ya Diwani wa kata ya Sola inayounda Mamlaka ya Mji mdogo Mh, Masanja Mpiga

Katika  kikao  hicho  Madiwani  walipata  nafasi  za  kuchangia  agenda  mbalimbali  ikiwemo  suala  la  Kusimamia  na  kuongeza  Mapato  ya   Halmashauri  ya  Maswa

Sauti za Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa wakiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani robo ya pili ya Mwaka wa Fedha 2023/ 2024