Sibuka FM

Maswa: Wakurugenzi wa Halmashauri Mkoani Simiyu watakiwa kutenga Bajeti ya Elimu ya watu wazima

27 September 2023, 8:11 am

Pichani:Mkuu wa Wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge akiwahutubia wananchi kwenye maadhimisho ya kilele cha siku ya Elimu ya watu wazima yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Nguzo 8 Wilayani Maswa.

Wasichana wapatao (222) Mkoani Simiyu wamefanikiwa kuendelea na masomo yao ya Elimu ya Sekondary Mbadala baada ya kujifungua.

Na Alex Sayi

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt,Yahaya Nawanda amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote Mkoani hapa kuhakikisha wanatenga bajeti kwa ajili ya kuendeleza Elimu ya watu Wazima wakati Serikali ikiaanda utaratibu wakuzihudumia Shule hizo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Maswa Aswenge Kaminyoge kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu wakati akiwahutubia wananchi kwenye maadhimisho ya kilele cha Elimu ya watu Wazima yaliyofanyika Septemba 25 mwaka huu Viwanja vya Nguzo 8 Wilayani Maswa.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge.

Lidia Joseph mwanafunzi mwenye mtoto mmoja anaeendelea na masomo ya elimu ya Sekondari mbadala Chuo cha maendeleo Malampaka Wilayani Maswa kati ya wasichana (22)waliopo Chuoni hapo amesema kuwa anamshukuru Rais Samia kwakuwapatia fursa hiyo yakujiendeleza tena kimasomo ili waweze kuzifikia ndoto zao.

Sauti ya Lidia Joseph

Akizungumza na Radio Sibuka Mkuu wa Chuo cha maendeleo Malampaka Michael Mahundi amesema kuwa chuo hicho kimekuwa na msaada mkubwa kwa wasichana hao kisaikolojia kwakuwa kinawaondolea hali ya unyanyapaa huku Chuo kikiwasaidia pia kusoma masomo ya Ufundi,hivyo huhitimu wakiwa wamemaliza masomo yao ya Sekondari na Elimu ya Ufundi kwa kipindi cha muda wa miaka miwili tu.

Mkuu wa Chuo cha Maendeleo Malampaka Michael Mahundi.
Pichani: Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo Malampaka Michael Mahundi

Ester Malwa Afisa Elimu ya watu Wazima,Elimu nje ya mfumo rasmi na Elimu maalum Mkoa wa Simiyu alisema kuwa Mkoa una jumla ya wasichana (222)waliokatisha masomo yao  kwa sababu ya ujauzito wanaoendelea na masomo yao katika vituo (8) chini ya mfumo wa elimu  ya Sekondari mbadala vilivyopo Mkoani hapa.

Baadhi ya Vijana wa Chuo cha Ufundi Malamapaka Maswa wakiwa kwenye moja ya mabanda yao wakionyesha baadhi ya fani wanazochukua ikiwa ni fani ya Umeme,Ufugaji na Ufundi wa Mfumo wa Maji.