Sibuka FM

96 wahitimu mafunzo ya udereva Maswa

1 March 2024, 8:07 pm

Pichani mwenye miwani ni Mkuu wa Wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge, kulia kwake ni Mwenyekiti wa Usalama Barabarani Samweli Mwanga, anayefuatia ni Mkuu wa Usalama barabarani Wilaya ya Maswa James Nyorobi na wa Mwisho mwenye shati ya Bluu ni Mkuu wa chuo cha Ufundi stadi Binza Mabula Daniel. Picha na Nicholaus Machunda

Jumla  ya  maafisa  usafirishaji 96  wamepatiwa  vyeti vya  udereva  na  leseni  za  uendeshaji  vyombo  vya  moto  ikiwemo  pikipiki  na  magari  madogo  baada  ya  kufuzu  mafunzo  ya  uendeshaji  wa  vyombo  hivyo.

Akikadhi  vyeti  hivyo  na leseni , Mkuu  wa  Wilaya  ya  Maswa  Mh  Aswege  Kaminyoge amesema  kuwa  alitoa  nafasi  hiyo  ya  kupata  mafunzo  bure  ya  uendeshaji   wa  vyombo  vya  Moto  ili  kupunguza  ajali  zisizo  za  lazima.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh Aswege Kaminyoge

Aidha  Mkuu  huyo  wa  Wilaya  ametoa miezi  Mitatu  kwa  Maafisa  Usafirishaji ambao  hawajapata   Mafunzo  wahakikishe  wanapata  Mafunzo na kupata  Leseni  itayomfanya  afanye  shughuli  zake  bila  kusumbuliwa  na  Askari  wa  Usalama  barabarani.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh Aswege Kaminyoge

Akitoa  taarifa  kwa   Mkuu  wa  Wilaya, Mkuu wa  chuo  cha  Ufundi  Stadi   Binza    Mabula  Daniel  amesema  kuwa  Wamefundisha   mambo  mbalimbali  ikiwemo  alama  na  Michoro  ya  Barabarani, Udereva  wa  Kijihami  na  Sheria  za  Usalama  Barabarani

Sauti ya Mabula Daniel Mkuu wa chuo cha Ufundi stadi Binza

Kwa  upande  wake   Kamanda  wa  Kikosi  cha  Usalama  Barabarani  Mkoa  wa  Simiyu  SSP   Namsemba  Mwakatobe amewataka  waendesha  vyombo  vya  Moto  waliopata  Mafunzo  kwenda  kuwa  Mabalozi  kwa  Wengine  kwenda  kusoma  ili  kupunguza  ajali  za  barabarani.

Sauti ya RTO Simiyu SSP Namsemba Mwakatobe

Yusuph  Mahega  ni  Mwenyekiti  wa  Waendesha  Boda  boda  Wilaya  ya  Maswa amemshukuru  Mkuu  wa  Wilaya   kwa  kutoa  Mafunzo  bure  kwa  maafisa  hao  huku  wakimuomba  asichoke  kuendelea  kuwasaidia.

Sauti ya Yusuph Mahega Mwenyekiti wa Bodaboda Wilaya ya Maswa
Waendesha bodaboda wilaya ya Maswa wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya wakati wa Kukabidhiwa Vyeti vya Mafunzo ya Udereva wa Pikipiki na Magari Madogo.