Sibuka FM

Maswa: Ummy afurahishwa uwekezaji binafsi sekta ya afya

14 July 2023, 11:21 am

Pichani: Waziri Ummy Mwalimu akiwa na mmiliki wa Barikiwa Dispensary Dkt,Hildegard Ashley Lucas akimwongoza kujionea uwekezaji kwenye Zahanati hiyo.Picha na Alex Sayi.

Waziri ahamasisha wawekezaji binafisi sekta ya Afya Mkoani Simiyu ili kusaidiana na Serikali huwahudumia wananchi Mkoania hapa.

Na,Alex Sayi.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amefurahishwa na uwekezaji binasfi kwenye Sekta ya Afya uliofanywa na mwekezaji binafsi Wilayani Maswa Mkoani Simiyu.

Ummy ameyasema hayo akiwa ziarani Wilayani Maswa Mkoani Simiyu alipotembelea kwenye Zahanati ya Barikiwa Dispensary kufuatia maombi ya mwekezaji huyo kuomba Zahanati hiyo ipande kiwango nakuwa kituo cha Afya.

“Serikali inakaribisha wawekezaji binafsi kwenye sekta ya Afya ili kusaidizana na Serikali kutoa huduma hii kwa wananchi na nimefurahishwa na uwekezaji huu,majengo mazuri na vifaa vya kisasa nadhani kunahaja ya zahanati hii kupewa kibari kuwa Hospital level one.”Amesema Waziri Ummy.

Pichani:Dkt,Ashley mmiliki wa Zahanati ya Barikiwa Dispensary akitolea ufafanuzi wa huduma zinazotolewa kwenye Zahanati hiyo kwa Waziri Ummy.Picha na Alex Sayi.

Akizungumza na Radio Sibuka Mkurugenzi wa Barikiwa Dispensary Dkt,Hildegard Ashley Lucas amesema kuwa anaishukuru Serikali ya Mama Samia na Waziri mwenye dhamana Ummy kwa kuthamini uwekezaji wake nakumpa ridhaa yakuomba kuwa Hospiatal na sio kituo cha Afya.

Sauti ya Dkt,Hildegard Ashley Lucas.