Sibuka FM

TARURA kutumia zaidi bil. 4.1 ukarabati wa miundombinu Maswa

21 March 2024, 7:05 pm

Pichani:Mhandisi wa Barabara Wilayani Maswa Mkoani Simiyu, Mhandisi Baraka Libungo akipitia nyaraka Ofisini kwake .Picha na Alex Sayi.

Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA)Wilayani Maswa Mkoani Simiyu wanatarajia kuzifanyia marekebisho Barabara zenye mtandao wa Km,227.21 zilizoathiriwa na Mvua za msimu.

Na. Alex Sayi

Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) imeendelea na matengenezo ya barabara zilizoathiriwa na mvua za msimu kwa lengo la kurejesha mawasiliano kwa Wananchi.

Hayo yamesemwa na Mhandisi wa barabara wilayani hapa Baraka Libungo kwa niaba ya Meneja (TARURA) Wilaya na kusema kuwa kwa sasa wamefikia (40%) ya matengenezo hayo.

Sauti ya Mhandisi wa Barabara Wilayani hapa Baraka Libungo

Libungo ameongeza kuwa matengenezo hayo yanagharimu zaidi ya Tsh. bil 4.1 kwa kujumisha shughuli za ujenzi wa  madaraja, mitaro, kuweka karavati, ujenzi wa kingo za madaraja, kuchonga na kuweka moramu kwenye  mtandao wa barabara wenye urefu wa Km. 227.21.

Sauti ya Mhandisi wa Barabara Wilayani hapa Baraka Libungo

Peter Mlyandingu Diwani wa kata ya Nguliguli wilayani hapa ameishukuru serikali kwa kuwa sikivu chini ya Meneja (TARURA) kwa kunusuru kwa wakati uharibifu wa miundombinu hiyo.

Sauti ya Diwani wa Nguliguli Peter Mlyandingu

Sayi Shola na Kija Samweli wakazi wa kijiji cha Mwashegeshi kata ya Ngulinguli wilayani hapa kwa nyakati tofauti wamezungumzia hali ya  uharibifu wa daraja la Mwashegeshi  na kusema kuwa inahatarisha usalama wa watumiaji huku akiiomba (TARURA) kuharakisha  ujenzi wa daraja hilo

Sauti za Wananchi Sayi Shola na Samweli Kija wakazi wa kijiji cha Mwashegeshi
Pichani:Sayi Shola Mkazi wa kijiji cha Mwashegeshi Kata ya Nguliguli Wilayani hapa akiangalia akiangalia hali ya Barabara iliyokuwa karibu kusobwa na Maji kwenye Daraja la Mwashegeshi.Picha Na,Alex Sayi.