Sibuka FM

Takukuru Simiyu yaokoa zaidi ya shilingi milioni 70

25 February 2024, 6:29 pm

Picha ya Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Simiyu Aron Misanga

Na Nicholaus Machunda

Taasisi  ya  Kuzuia  na  Kupambana  na  Rushwa  mkoa  wa  Simiyu  imefanikiwa  kuokoa  fedha   zaidi  ya shilingi  milioni sabini  zilizotaka  kufanyiwa  ubadhirifu  katika  Chuo cha  Maafisa  Tabibu  wilayani  Maswa.

Akitoa  taarifa  kwa  waandishi  wa  habari, Naibu Mkuu wa  Takukuru  mkoani  hapa   Aron   Misanga   amesema  kuwa  fedha  hizo  zilipelekwa  chuoni  hapo  kwa  ajili  ya  posho  ya  kazi  maalum iliyofanyika  lakini Takukuru  ilipofuatilia  ilibaini  kuwa  wahusika  hawakupewa  fedha  zao.

Sauti ya Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Simiyu Aron Misanga

Aidha   Naibu  Mkuu  wa  Takukuru  amesema  kuwa  wamefanya  ufuatiliaji  katika  ukusanyaji  wa  mapato  kwa  mfumo  wa  POS  katika halmashauri  ya  Maswa  pamoja  na  ununuzi  wa  pamba  kupitia  Amcos  ya  mbalimbali mkoani  hapa   na  kugundua  ubadhirifu  mkubwa  uliokuwa  umefanyika.

Sauti ya Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Simiyu Aron Misanga

Katika  uchambuzi  wa  mfumo  Takukuru  mkoa  wa  Simiyu  ilibaini  mapungufu  makubwa  katika  utoaji wa  huduma  katika  Idara  ya  Ardhi  hali  inayopelekea  kuwepo  kwa mianya  ya  rushwa.

Sauti ya Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Simiyu Aron Misanga

Takukuru  mkoa  wa  Simiyu  inatoa  wito  kwa   wananchi  kuendelea  kushirikiana  na  serikali  pamoja  na utoaji  wa  taarifa  za  rushwa  na ubadhirifu  wa  fedha  za  miradi inayoendelea  kujengwa.

Sauti ya Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Simiyu Aron Misanga