Sibuka FM

MKAKATI WA KUTAMBUA MAMA WAJAWAZITO WOTE KUPITIA DATARI MAALUMU WALETA MATOKEO CHANYA WILAYANI MASWA..

26 September 2022, 11:47 am

Mkakati  wa  kutambua wajawazito Wilayani  Maswa  umeleta mabadiliko  makubwa ikiligaishwa  na  hapo  awali ambapo  wajawazito walikuwa hawatambuliki hali iliyokuwa inapelekea  baadhi yao kujifungua  majumbani na kuhatarisha  Maisha  yao.…

Hayo  yamesemwa  na  Mkuu  wa  Wilaya  ya  Maswa  Mh  Aswege  Kaminyoge   wakati  akitoa  Elimu  kwa  Wananchi  kupitia  Radio  Sibuka  fm  na  Kusema  kuwa   Mkakati  huo umekuwa  na Manufaa makubwa  ya kupunguza  vifo  vitokanavyo  na  Uzazi.

“Nipede  tu  kutoa  Ushuhuda  kwamba  Mkakati tuliokuja  nao  kama  Wilaya  ya  Maswa  kuhakikisha  Akina Mama  wajawazito  wote  wanatambuliwa na  kuwekwa  kwenye Daftari maalumu ili  kurahisisha  Ufuatiliaji  wa  Maendeleo ya Ujauzito  wao “..

 “Mkakati  huu  umefanya idadi  ya  Wanaojifungulia kwenye   Vituo vya  Kutolea  Huduma za  Afya kuongezeka ikilinganishwa  na  kipidi  kile  hatujawa  na  Mkakati  huu  ambao  lengo  lake  ni  zuri  tu  na  liasaidia  sana  wataalamu  wa  Afya  kufatilia  mwenendo  wa  mama  mjamzito  na  Changamoto  zake “ ..          

Akizungumza  na  Sibuka  Fm  Radio katika  mahojiano  maalumu  Mratibu  wa  Huduma  ya  Afya  ya   Baba,  Mama  na  Mtoto   wilaya  ya  Maswa  Dokta   Angella  Ngaiza  amesema  kuwa  idadi  ya  akina mama Wajawazito wanaojifungulia  kwenye  vituo vya  Afya  imeongezeka  hadi  kufikia  Asilimia  91.4 % .”

“Kwakweli  tuapokea  akina mama  Wengi  sana  wanaokuja  kujifungulia  kwenye  Vituo  vyetu  vya  Afya  hii  nikutokaa  na  Mkakati  tulioanzisha  wa  kuwa  a  Daftari  Maalumu  la  kutambua wajawazito Jambo  linalotutia  Moyo sisi  wahudumu “

“ Pia  niwashukuru  sana  Radio  Sibuka   kwa  nafasi  mnayotupatia  ya  Airtime  bure  kwa  ajili  ya  kuwahabarisha  wananchi  wetu  kuhusu  Masuala  ya  Afya  ikiwemo  haya  ya  kujifungulia  kweye  vituo  vya  Afya  ndio  maana  idadi  imeongezeka  sana”