Sibuka FM

DC Maswa aonya  wanaohujumu miundombinu ya maji

16 November 2023, 8:22 pm

Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Aswege Kaminyge akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Seng’wa

Na Nicholaus Machunda

Mkuu  wa wilaya  ya  Maswa mkoani  Simiyu   Mh,  Aswege  Kaminyoge  ameonya wananchi  wanaohujumu miundombinu ya maji  yanayotoka  Ziwa Viktoria  kuja  kata  ya Sengwa  iliyopo wilayani   hapa  kupitia wilaya ya Kishapu.

Mh  Kaminyoge  amesema  hayo  wakati Kamati  ya  Ulinzi  na  Usalama  ya wilaya ilipotembelea mradi  huo ambao  umekuwa ukihujumiwa  mara  kwa  mara  na  wananchi  kwa  kupasua  bomba la maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu na kunyweshea  mifugo  yao..

Sauti ya DC Maswa Aswege Kaminyoge

Aidha   Mh  Kaminyoge   amesema  kuwa   tayari  ameshachukua   hatua   ya  kuwasiliana   na  Mkuu   wa  Wilaya  ya  Kishapu  ili  kuweka   namna   nzuri  ya  wananchi   hao  kujengewa   vituo  vya  kichotea   maji  na  kunyweshea   vifugo  yako  ili   wasiendelee   kuharibu  miundombinu hiyo.

Sauti ya DC Maswa Aswege Kaminyoge akiongea na Wananchi wa Seng’wa

Akitoa  taarifa  ya  Utekelezaji  wa   Mradi   huo Meneja  wa   Wakala wa  Maji na  Usafi  wa  Mazingira  vijijini  (RUWASA)  Wilaya  ya Maswa   Mhandisi  Lucas  Madaha  amesema  kuwa   kumekuwepo  na  adha  ya  Wananchi   wa  Sengwa kukosa  maji  kutokana  na  kutobolewa   kwa  bomba  hilo..

Sauti ya Meneja RUWASA Wilaya ya Maswa Mhandisi Lucas Madaha

Mhandisi   Madaha   ameongeza  kuwa  katika  mwaka  wa  Fedha  Ujao  RUWASA  imepanga kuongeza  mtandao  wa  Maji   ili  vijiji   vyote   vya  kata   ya  Sengwa   vipate  huduma  ya Maji  ya kutoka ziwa viktoria.

Sauti ya Meneja RUWASA Wilaya ya Maswa Mhandisi Lucas Madaha

Baadhi  ya  Wananchi   wa  kijiji  hicho  Wameishukuru Serika  kwakuwaletea  mradi huo  huku wakiiomba  Serikali  kuwachukulia   hatua  Wananchi  wanaohujumu  Miundo mbinu  ya  maji  hali  inayopelekea  wananchi  wengi  kukosa  maji.

Baadhi ya Wananchi wa kata ya Seng’wa wakizungumzia changamoto ya Maji