Sibuka FM

Waandishi Redio Jamii wapigwa msasa ushindani habari za mtandaoni

4 July 2023, 5:18 pm

Mkufunzi mafunzo ya Editorial Radio Portal toka (TADIO) Amua Rushita akiteta neno na waandishi wa habari. Picha na Alex Sayi.

Na,Alex Sayi

Waandishi wa habari na wahahiri wa Redio  Jamii mikoa ya Kanda ya Ziwa wameshauriwa kuendana na mabadiliko ya uandaaji wa habari zenye ushindani kwenye mitandao ya kijamii.

 Paschal Malulu mshiriki wa mafunzo toka Kahama Shinyanga amezungumzia umuhimu wa mafunzo hayo yaliyofanyika Gold Crest Hotel nakusema  kuwa mafunzo hayo yamepanua uelewa kwa Waandishi ili kwendana na ulimwengu ulipo kwa sasa kwakuwa kwa sasa habari zimeridi kiganjani

Paschal Malulu akizungumzia faida za mafunzo hayo

kwa sasa habari zimeridi kiganjani

Zaituni  Juma  mshiriki na Mwandishi toka mkoani Tabora amesema  kuwa mafunzo hayo yatawasaidia waandishi  kuandaa habari zinazoweza kuwafikia watu wengi zaidi walio nje ya mikoa husika.

Zaituni Juma Mshiriki toka Tabaro akizungumzia faida ya mafunzo hayo.

Kwa upande wake Amua Rushita  mkufunzi toka Tanzania Development Information Organazatio(TADIO) amesema kuwa matumizi ya habari za mitandaoni umesaidia Radio za kijamii kuongeza wigo wa wasikilizaji walio nje ya mikoa yao.

Akizungumza wakati wa uhitimishaji wa mafunzo hayo Bi,Joan Kanza Afisa tathmini na ufuatiliaji mafunzo toka (TADIO) amesema kuwa mafunzo hayo yanajumuisha waandishi zaidi ya (25) toka Radio za kijamii Kanda ya Ziwa na kuongeza kuwa hadi sasa (TADIO) inahudumia zaidi ya redio (43) za kijamii nchini.