Sibuka FM

Taasisi  ya  TWAWEZA  yatoa  Mafunzo   Kwa  Waraghabishi  Wilayani  Maswa.

22 February 2022, 6:02 pm

Jumla  ya  Waraghabishi  Thelathini  na  sita (36)  kutoka  kata  18  za  wilaya  ya  Maswa  Mkoani  Simiyu  wamepewa  Mafunzo  ya  kuwawezesha  kuibua   changamoto  na  Vipaumbele  vya  Maendeleo  kwenye   maeneo  ya  vijiji  vyao.

Akizungumza  na  Sibuka  Fm   Meneja  Programu  kutoka  Shrika  la  Kawie  Social Development  Foundation (KASODEFO)   Marius  Isavika  amesema  kuwa  lengo  la  kukutanisha  Waraghabishi  hao  ni  kupitia  Changamoto  zilizoibuliwa  katika  kipindi  cha Utafiti Shirikishi   kwa  Wananchi..

Sauti ya Marius Isavika- KASODEFO

             

Isavika  amesema  kuwa  wanalenga  kufika  kata  zote  za  wilaya  ya  Maswa  ambapo  ndipo  Mradi  huo  unatekelezwa   ili  waanchi  wawe   na  Uwezo  wa  Uibua  na  Kubaina  Changamoto  zinazowakabili  na  kuzitafutia  Ufumbuzi..

Sauti ya Marius Isavika- KASODEFO

           

Rukia  Masanyika  ni  mwezeshaji  kutoka  Taasisi  ya  TWAWEZA   amesema  kuwa  Uraghabishi  ni  Dhana  ambayo  inalenga  kusaidia  wana Jamii  kuibua  hoja   zao  wenyewe ..

Sauti ya Rukia Masanyika – TWAWEZA

              

Nao  baadhi  ya  Wadau   na  Washriki  wa  Mafunzo  hayo  wamesema  kuwa wamejifunza  mbinu mbalimbali  za  kushirikisha  Jamii  katika  kuimbua  Masuala  mbali  ya  maendeleo..

Baadhi ya Sauti za Wadau na Washiriki wa Mafunzo.

            

Hapa chini ni Baadhi ya Picha za Washiriki wakiwa katika Mafunzo ya Uraghabishi.