Sibuka FM

Mei 30 mwaka huu historia ya umeme inaenda kuandikwa Simiyu

17 April 2026, 4:26 pm

Pichani ni mkurugenzi mtendaji wa TANESCO nchini,Lazaro Twange akizungumza na waandishi wa habari hawapo kwenye picha baada ya kumaliza kujionea maendeleo ya mradi wa kituo cha kupozea umeme mkoani Simiyu Picha kutoka maktaba ya Sibuka fm

Tunahitaji kuwa na umeme wa uhakika ambao hauwezi kuwa kikwazo hasa kwa wafanyabiara na wajasiriamali ambao shughuli zao zinahitaji nishati hiyo bila kukatika mara kwa mara ili waweze kujiongezea kipato zaidi”.

Na,Daniel Manyanga 

Wakazi wa mkoa wa Simiyu wameiomba serikali kupitia shirika la umeme Tanzania TANESCO kuhakikisha ahadi ya kupata umeme wa uhakika ifikapo Mei 30 mwaka huu inatekelezeka ili kuepusha usumbufu ambao wamekuwa wakiupata wa kukatika mara kwa mara kwa huduma hiyo muhimu hivyo kupelekea kuunguziwa kwa baadhi ya vifaa vyao vinavyotumia umeme. 

Wakizungumza na Sibuka Fm,Antony John ambaye ni mchomeleaji na Hamza Kipala ambaye ni kinyozi wamesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutawawezesha kufanya zao bila kuwa na hofu na hivyo kujiongezea kipato zaidi.

Sauti ya wananchi

Mradi huo unatekelezwa na wahandisi kutoka shirika la umeme Tanzania (TANESCO) chini ya idara ya usafirishaji wa umeme na tayari umefikia asilimia 46 za utekelezaji wake kama anavyofafanua hapa mhandisib,Daniel Kato msimamizi wa mradi huo

Sauti ya msimamizi wa mradi huo

Lazaro Twange ni mkurugenzi mtendaji wa TANESCO amesema kuwa changamoto ambazo zinawakumba wakazi wa mkoa huu zinatarajiwa kuisha mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho cha kupozea umeme

Sauti ya mkurugenzi mtendaji wa TANESCO

Mbali na ujenzi wa kituo hicho mkurugenzi huo ametoa wito kwa wale ambayo wanadaiwa kuhakikisha wanalipa ili kuepuka kusitishiwa huduma hiyo.

Sauti ya Lazaro Twange akihimiza wadaiwa kulipa madeni ili kuepuka kusitishiwa kwa umeme