Sibuka FM

Homa ya mapafu yatishia usalama wa mifugo Maswa

23 April 2024, 8:58 am

Pichani ni mmoja wa maafisa mifugo wilayani Maswa akiendelea na zoezi la uchanjaji wa ng’ombe Picha na Paul Yohana

Zoezi la uchanjaji wa mifugo wilayani Maswa mkoani Simiyu  kuwasaidia wafugaji kufanya ufugaji wenye tija na kuongeza thamani ya mifugo yao hivyo kuondokana na umasikini.

Na,Paul Yohana

Zaidi ya ng’ombe laki tatu wilayani Maswa mkoani Simiyu kupatiwa chanjo ya homa ya mapafu ili kukabiliana na ugonjwa huo ambao unaenea kwa kasi hali inayopelekea kufungwa kwa baadhi ya minada na kuwatia umasikini wafugaji.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Maswa, Paulo Maige wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji wa chanjo ya homa ya mapafu kwa ng’ombe lililofanyika kijiji cha Mwanh’egele kata ya Nyabubinza wilayani hapo.

Sauti ya mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Maswa akizungumza wakati wa zoezi la chanjo

Samwel Nyalandu ni katibu wa chama cha wafugaji wilayani hapo amesema kuwa wafugaji wanakabiliwa na changamoto za malisho,maji na masoko huku akiwaomba wafugaji kujiunga na chama hicho ili waweze kunufaika na mikopo inayotolewa na benki bila kuwa na mashariti magumu.

Sauti ya katibu wa chama cha wafugaji wilayani hapo akiwaomba wafugaji kujiunga na chama hicho

Kwa upande wake daktari wa mifugo wilaya hapo Dkt.Charles Masila akisoma ripoti mbele ya mwenyekiti wa halmashauri hiyo amesema kuwa wamekusudia kuchanja ng’ombe zaidi ya laki tatu ili kuweza kuikinga mifugo na homa ya mapafu ambao umeonekana kukua na kusambaa kwa kasi na kusababisha vifo kwa mifugo hali inayosababisha kufungwa kwa baadhi ya minada.

Sauti ya daktari wa mifugo akizungumzia faida ya chanjo hiyo kwa mifugo

Akizungumza kwa niaba ya wafugaji, Malale Mbizo amesema kuwa serikali inapaswa kuendelea kutoa chanjo hizo ili kuikinga mifugo na magonjwa kama hayo.

Sauti ya mmoja wa wafugaji akiomba serikali iendelee na chanjo za mifugo kwenye magonjwa mengine