Sibuka FM

Mfumo wa stakabadhi ghalani kuwanufaisha wakulima Simiyu

16 April 2024, 10:04 am

 

Mifuko ya Choroko ikiwa katika ghala zikiwa zimeuzwa kwa mfumo wa Stakabadhi ghalani

Na Nicholaus Machunda

Wakulima Mkoani Simiyu wapata mwarobaini wa bei ya mazao baada ya kilio cha muda mrefu cha kukosa soko la uhakika

Wananchi  Mkoani  Simiyu  Wameishukuru  Serikali  Kuruhusu  kuuza  Mazao  yao  ya  Nafaka  kupitia  Mfumo  wa  Stakabadhi  Ghalani  kuwa  Umekuwa  na  faida  kwao  huku  ukilenga   kumkomba  Mkulima.

Laurensi   Masunga  Chajo  ni  Mkulima  kutoka  Wilaya  ya  Meatu  Mkoani  hapa  amesema   kuwa  mfumo  huo  ni  mzuri  kwani  unafaida  kwa  Mkulima   na  utamkomboa  kiuchumi

Sauti ya Mkulima akizungumzia alivyonufaika

Kwa Upande  wake  Japheti Magulyati  ni  Mkulima  kutoka   Maswa  anaishukuru  Serikali  kwani  mfumo  huo  umewanufaisha  zaidi  ikilinganishwa  na  hapo  awali  ambapo  bei  ya  choroko  ilikuwa  haieleweki

Sauti ya Mkulima akizungumzia alivyonufaika na Mfumo huo

Akitoa  Ufafanuzi  juu  ya Bei ya  Mnada  katika  Zao  la  Choroko  na  Faidi  watakayopata  Wakulima  kupitia  Bei  hiyo,  Mwenyekiti  wa  Chama  Kikuu  cha  Ushirika  Mkoa  wa  Simiyu  (SIMCU)    Ndugu  Lazaro  Walwa  amesema  bei  ya  Ushindanishi  ni   nzuri  na  Faida  inayopatikana  inarudi  kwa  Wakulima

Sauti ya Lazaro Walwa Mwenyekiti wa SIMCU
Pichani ni Mwenyekiti wa SIMCU Ndugu Lazaro Walwa akielezea Manufaa na Bei waliyouza mazao

Aidha  ndugu  Walwa  ametoa  rai  kwa  Wakulima   kupeleka  Choroko  kwenye  vyama  vya  Msingi  vya  Ushirika  (AMCOS )  kwani  kuna  tofauti  kubwa  kati  ya  Bei  ya  Mtaani  na  Bei  ya  Mfumo  wa  Stakabadhi  Ghalani

Sauti ya Lazaro Walwa Mwenyekiti wa SIMCU