Sibuka FM

Maswa: Ng’ombe 126, kondoo 68 sadaka ya kuchinja Eid Al Hajj

1 July 2023, 3:54 pm

Kwenye picha ni Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu(BAKWATA) wilayani Maswa, Maulid Mlete mwenye kanzu akimkabidhi Bi.Salima Kimazi sadaka ya nyama ya ng’ombe wakati wa utoaji wa sadaka ya kuchinja katika kusherekea sikukuu ya Eid Al Hajj

Na Mwandishi, Daniel Manyanga

Baraza Kuu wa Waislamu nchini Tanzania (BAKWATA)  wilayani Maswa mkoani Simiyu kwa kushirikiana na Taasisi ya Tabasamu Tanzania Foundation iliyopo mkoani Shinyanga wametoa sadaka ya kuchinja  ng’ombe 126 na kondoo 68 katika kusherehekea sikukuu ya Eid Al Hajj kwa wananchi wilayani Maswa.

Hayo yamesemwa na katibu wa Taasisi ya Tabasamu Tanzania Foundation Mussa Shusha wakati wa zoezi la utoaji wa sadaka hizo lililofanyika Julai Mosi katika mnada wa Maswa uliopo kata ya Nyalikungu kitongoji cha Mnadani.

Shusha amesema kuwa taasisi hiyo imajihusisha na Ujenzi wa Misikiti,Madrasa,Uchimbaji wa Visima na mahitaji mbalimbali kwa kuzingatia umuhimu na uhitaji wa sehemu husika bila kujali Dini wala Kabila ambapo kwa mwaka huu wamefanikiwa kutoa sadaka ya kuchinja ng’ombe 4000 mkoani Shinyanga.

Sauti ya Katibu wa Tabasamu Tanzania Foundation ,Mussa Shusha

Shusha ameongeza kuwa wananchi wa Tanzania wanauhitaji mwingi sana katika maeneo wanayoishi hivyo kama Taasisi wataendelea kutoa misaada kadri ya uwezo wao na kuziomba Taasisi zingine ziweze kuisadia jamii yenye uhitaji.

Sauti ya Katibu wa Tabasamu Tanzania Foundation ,Mussa Shusha

Akizungumzia Sadaka hiyo iliyotolewa na Taasisi ya Tabasamu Tanzania Foundation ,Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) Wilaya ya Maswa,Maulid Mlete ameishukuru Taasisi hiyo kwa Sadaka ya Kuchinja na kuziomba taasisi zingine ziweze kuiga mfano huo kwa kufuata utaratibu unaotakiwa ili kuondoa taharuki kwa wananchi.

Sauti ya Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu(BAKWATA) wilaya ya Maswa,Maulid Mlete

Kwa upande wake baadhi ya wananchi walichukua sadaka hiyo wakawa na haya ya kuzungumza.

Sauti ya Wananchi Shija Sanane & Salima Kimazi