Sibuka FM

DC Maswa: Wananchi tunzeni vyanzo vya maji

16 December 2023, 12:01 pm

This image has an empty alt attribute; its file name is img-20231215-114138-276-1024x450.jpg
Pichani: Katikati mwenye Suti ni Mkuu wa wilaya ya Maswa Mhe.Aswege Kaminyoge,kulia kwake ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mhe.Paul Maige mwenye kaunda suti na tatu kutoka kulia kwa mkuu wa wilaya ni Meneja wa RUWASA wilaya ya Maswa Mhandisi.Lukas Madaha na kutoka upande wa Kushoto wa mkuu wa wilaya ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa,Maisha Mtipa mwenye Tshit nyeusi wakiwa kwenye picha ya pamoja katika mkutano wa wadau wa maji Picha na Daniel Manyanga

Wadau wa maji na Wananchi watakiwa kutunza vyanzo vya maji ili kuweza kukabiliana na ukame unaosababishwa na shughuli za kijamii pamoja na mabadiliko ya tabia nchi

Na Daniel Manyanga

Mkuu wa Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu Mhe.Aswege Kaminyoge amewataka Wananchi na Wadau wa Sekta ya Maji Wilayani hapo kutunza vyanzo vya Maji Ili kukabiliana na ukame unaosababishwa na shughuli za kijamii pamoja na Mabadiliko ya tabia  nchi.

Kaminyoge ametoa Rai hiyo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mwaka wa Wadau wa Sekta ya Maji ulioandaliwa na wakala wa Maji na usafi wa Mazingira Vijijini  Wilayani hapo (RUWASA) uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya hiyo.

Kaminyoge amesema kuwa kumekuwepo na tabia za baadhi ya watu kufanya shughuli za kijamii katika vyanzo vya Maji hali ambayo inapelekea Kuua vyanzo  hivyo hasa mto Sola unaotegemewa  kujaza bwawa la New Sola ambalo ni Chanzo Kikuu Cha Maji mjini hapo na kuwaomba wadau wa maji kuendelea na zoezi la upandaji wa miti, kuacha shughuli za kijamii katika vyanzo hali ambayo itasaidia kutunza vyanzo vya maji wilayani hapo.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe.Aswege Kaminyoge akizungumza na wadau wa maji katika mkutano wa mwaka ulioandaliwa na RUWASA

Kaminyoge ameongeza kuwa  Kuna baadhi ya  Viongozi wa kisiasa na Wananchi  wamekuwa ni sehemu ya kuhujumu miundombinu ya maji ambayo tayari inafanya kazi hivyo amewataka kuachana na tabia hizo na badala yake Wadau wa Maji,Viongozi na Wananchi wawe sehemu ya kulinda miundombinu hiyo ili iweze kunufaisha hata vizazi vijavyo.

Mkuu wa Wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge akiwataka wadau wa maji kuacha kuhujumu miundombinu ya maji

Awali meneja wa RUWASA wilaya ya Maswa Mhandisi.Lukas Madaha amesema kuwa kuanzia mwaka 2019 mwezi Julai wametekeleza miradi mbalimbali ya Maji yenye jumla ya fedha zaidi bilioni 8 hali ambayo imepelekea kuongeza upatikanaji wa maji vijijini hadi kufikia asilimia 74.

Sauti ya Meneja RUWASA wilaya ya Maswa Mhandisi.Lukas Madaha akiwasilisha mada katika mkutano wa mwaka wa wadau wa maji

Betty Isaack ni Mratibu wa shirika lisilokuwa la kiserikali la World Vision Mradi wa Shishiyu AP Amesema kuwa World Vision kama Mdau muhimu wa Maji wamechimba visima virefu vitatu katika mradi wa World Vision Shishiyu unaonufaisha wananchi zaidi ya elfu nne na mwaka wa fedha 2023/24 wamepanga kutumia zaidi ya milioni mia moja na thelathini kusambaza maji katika vitongoji na vijiji ambavyo havikuweza kupata maji kwa awamu iliyopita katika kata ya Shishiyu.

Sauti ya Mratibu wa World Vision Shishiyu Betty Isaack akiwasilisha mada katika mkutano wa mwaka wa wadau wa maji
Pichani: Aliyesimama ni Bi.Betty Isaack Mratibu wa World Vision Mradi wa Shishiyu akiwasilisha mada katika mkutano wa mwaka wa wadau wa maji wilayani Maswa Picha