Sibuka FM

LAAC yaipongeza Maswa kwa usimamizi mzuri wa miradi

28 March 2024, 10:19 am

Mwenye Suti nyeusi ni Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali -LAAC Mh Stanslaus Mabula akiwa anapata maelezo kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Maswa Dr James Bwire (Mwenye Koti Jeupe) na DMO Dr Hadija Zegega (Mwenye koti la drafti) Wakati wa kutembelea Jengo la Wagonjwa wa Dharura
Picha na Nicholaus Machunda

Kamati  ya  Kudumu  ya  Bunge  ya  Hesabu  za  Serikali  za  Mitaa –  LAAC   imeipongeza  Halmashauri  ya  Wilaya  ya  Maswa  kwa  Usimamizi  Mzuri  wa  Fedha  za  Miradi  ya  Maendeleo zinazoletwa  Wilayani  hapo.

Akitoa  Pongezi  hizo  mara  baada  ya  kutembelea  Jengo  la  Wagonjwa   wa   Dharura katika  Hospitali  ya  Wilaya  ya  Maswa   Mjumbe  wa  Kamati  hiyo   Mhe,    Suma  Fyandomo  amesema  kuwa   Jengo  hilo  ni la  kisasa kabisa   ukilinganisha  na  Majengo  mengine  ya  Dharura  waliyotembelea  katika  maeneo  mbalimbali.

Sauti ya Mhe, Suma Fyandomo-Mjumbe wa kamati ya LAAC

Akitoa  taarifa  kwa  Kamati  ya  Kudumu ya  Bunge  ya  Hesabu  za  Serikali  za  Mitaa  kuhusu  Ujenzi  wa  Mradi   wa   Jengo  la  Wagonjwa  wa  Dharura   Mganga  Mfawidhi  wa   wa  Hospitali  ya  Wilaya  ya  Maswa  Dr  James  Bwire  amesema  kuwa   Jengo  hilo  limekuwa  Msaada  mkubwa  katika  Utoaji  wa  Huduma  za  Dharura  kwa   wagonjwa

Sauti ya Dr James Bwire – Mganga Mfawidhi Hospitali ya Wilaya ya Maswa
Baadhi ya Vifaa vya kutolea Huduma katika Jengo la Wagonjwa wa Dharura

Kwa  Upande  wake   Makamu  Mwenyekiti  wa  Kamati  ya  LAAC   Mhe,   Stanslaus  Mabula  amesema  kuwa  Mradi  wa  Kiwanda  cha  Chaki  ni  wakipekee  sana  kwa  Ukanda  huu  hivyo  shauku   ya  Serikali  na  Watanzania  nikuona  Mradi  huu  unaleta  Manufaa  huku  akitoa  mwezi  Mmoja  ili  uanze  kufanya  kazi.

Sauti ya Makamu mwenyekiti wa LAAC Mhe Stanslaus Mabula

Baadhi  ya  Wananchi  Wilayani  hapa   wameishukuru  Serikali  kwa  kujenga  Jengo  hilo  ambalo  limesogeza  huduma kwani    hapo  awali  walikuwa  wakipa  shida kupeleka   Wagonjwa  Hospitali ya  kanda  ya  Bugando  na  Kutumia  Gharama  kubwa .

Sauti za baadhi wa Wananchi wa Wilaya ya Maswa

Naye  Mwenyekiti  wa  Halmashauri  ya  Wilaya  ya  Maswa  Mhe, Paul  Maige  amemshukuru  Rais  Samia  kwakuleta  Fedha  nyingi  kwa  ajili  ya  Utekelezaji    wa  Miradi  hiyo  ya  Kimkakati  huku  akiahidi  kutekeleza     Ushauri   wote  uliotolewa  na  Kamati  hiyo  ya  LAAC   mara  baada  ya  kutembelea    Jengo  la  Wagonjwa  wa  Dharura  katika  Hospitali  ya  Maswa  na  Ujenzi  wa  Kiwanda  cha   Chaki.

Sauti ya Paul Maige -Mwenyekiti wa Halmashauri ya Maswa
Wajumbe wa kamati ya LAAC wakiangalia chumba maalumu cha kuongozea Hewa ya Oksijeni